CWT wafunguka kuhusu tuhuma za Ufisadi zilizoandikwa kwenye gazeti la Jamuhuri


Na.Enock Magali,Dodoma

Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa ufafanuzi juu ya kile kilicho andikwa katika gazeti la JAMUHURI la tarehe 28 ya mwezi May,katika  ukurasa wake wa  mbele,iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho  Ufisadi ,Upendeleo  Chama cha walimu.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini dodoma, Rais wa Chama hicho Leah Ulaya,amesema kuwa  taarifa iliyochapishwa  kwenye gazeti hilo,haziendani  na  uhalisia  wa kile kinacho fanyika ndani  ya chama hicho  kwa sasa.

"Tunafata taratibu,kanuni na sheria zetu kulingana na katiba yetu ya CWT na chama chetu kitaendelea kuwa rafiki wa waandishi wa habari na vyombo vya habari vinavyozingatia misingi,weledi na taaluma ya habari,na tunategemea sana ushirikiano wenu katika kufikisha ujumbe kwa kadri tutakavyo wahitaji," Alisema.

Aidha, ameongeza kuwa habari hiyo kwa namna moja ama nyingine, ilikuwa na lengo la kuwafedhehesha, na pia  kukichafua chama hicho, pamoja na uongozi mzima wa Chama cha Walimu Tanzania sambamba na walimu wote hapa nchini.

Katika hatua nyingene Bi.Ulaya amesema kuwa,gazeti hilo lilichapisha hoja mbalimbali  ambazo wao kama CWT, wanaamini zimeandikwa bila kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa lengo la, kuiaminisha jamii ambayo ukiangalia kichwa cha habari hiyo, hakiendani na maudhui yaliyo andikwa ndani yake, ambapo mpaka sasa hawajui lengo la mwandishi wa habari hiyo,ilikuwa ni nini.

Mbali na hilo amesema gazeti hilo, limewatuhumu pia  katibu Mkuu na mweka hazina wa chama, kwa kile kinachodaiwa  kuwa walienda nchini Cape Verde, kuangalia mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na timu ya Taifa ya nchi hiyo Cape Vede kwa kutumia fedha za chama.

"Nasema hili kwa kuwa ili uweze kupata taarifa kamili ni lazima ukutane na uongozi mzima,na ofisi ya Makao makuu ya CWT,kwa kufanya hivyo tutakuwa tunahimarisha taaluma yenu kama waandishi wa habari na tutakuwa tunapeleka ujumbe sahihi kwa wananchi hususa ni wanachama wa CWT.Aliongeza.

Kwa upande wake, Deus Seif ambaye ni Katibu mkuu wa chama wa Chama hicho yeye amesema kuhusu madai ya kuajiri kwa upendeo,taratibu zote zilifuatwa,

from MUUNGWANA BLOG

Comments

Popular posts from this blog