Watanzania 100,000 walinda amani nchi za Afrika


Idadi ya Watanzania wanaofanya shughuli za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali imefikia 100,000 huku 3800 wakiwa wamepoteza maisha tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kutoa walinzi mwaka 1948.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi jijini Dare s Salaam katika siku ya kuwakumbuka na kuwapongeza walinzi wa amani katika nchi mbalimbali.

"Idadi walinda amani karibu 100,000 sasa hivi wako katika nchi mbalimbali za Afrika, hivyo tunawapongeza kwa kazi nzito waliyonayo lakini pia kuwakumbuka walinzi 3,800 waliopoteza maisha kuanzia mwaka 1948 tangu ilipoanza kazi ya ulinzi wa amani,"alisema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi alisema Tanzania ina jukumu la kulinda amani, ndio maana inawajibika kuwapeleka walinzi katika nchi mbalimbali ili kuwalinda raia wasiokuwa na hatia wanaotaabika na kukosa amani katika nchi zao.

Alizitaja baadhi ya nchi ambazo kwa sasa Tanzania imepeleka walinzi wa amani kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Afrika ya Kati, Lebanon na Sudan na kwamba bado Tanzania inaendelea kuwapeleka kila itakavyokuwa ikihitajika na Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuioyesha dunia kama nchi iko tayari kutoa msaada hasa itakapohitajika lengo likiwa ni kuifanya dunia maeneo salama kwa ajili ya watu kuishi.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema operesheni ya UN ya ulinzi wa amani ni uwekezaji wa amani na ulinzi kidunia.




from MUUNGWANA BLOG

Comments

Popular posts from this blog