DC aagiza kila Mwananchi kudhibiti mimba kwa Wanafunzi
Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Ally Kasinge ameagiza kila mwananchi kuhakikisha anashirikiana na serikali kudhibiti mimba kwa wanafunzi katika wilaya hiyo kutokana na takwimu ya wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni kuendelea kuongezeka.
Kasinge ametoa agizo hilo katika kikao cha cha tathmini ya elimu kilichofanyika wilayani hapo mara baada ya kusomewa takwimu za idara ya elimu zilizobainisha wanafunzi 22 kukatishwa masomo mwaka jana huku kuanzia januari 2019 hadi sasa wanafunzi 6 wakikatishwa masomo yao.
"Uwe kiongozi,uwe mwananchi,uwe mchungaji,uwe mwalimu,uwe askari lazima tuhakikishe tunafanya kazi ya kudhibiti mimba ya wanafunzi wa kike katika wilaya yetu, kila mtu mtu atimize wajibu wake na kwenye hili hatutamuacha mtu endapo haya yakiendelea,takwimu hizi mmeziona"alisema Kasinge
Kwa mujibu wa takwimu za idara ya elimu Zilizotolewa na Maofisa elimu sekondari na Msingi Akiwemo Loice Mgonja na Fredrick Mhanze wilayani humo imebainisha wanafunzi 22 walikatishwa masomo mwaka jana huku kuanzia januari 2019 hadi sasa wanafunzi 6 wamekatishwa masomo huku pia kuhusu utoro ikielezwa wanafunzi 166 hawakuripoti shule 2018 na wanafunzi 187 kwa 2019 jamno ambalo linaisukuma serikali kuchukua hatua .
"changamoto ya wanafunzi kupata mimba ni kubwa,hatua ambazo zinachukuliwa kwa sasa ni kila mmoja kwenye eneo lake amepewa jambo la kufanya ili lengo letu la kupambana na tatizo hili lifanikiwe" alisema mmoja wa maafisa elimu
baadhi ya wadau wa elimu ambao wameshiriki katika kikao cha cha tathmini ya elimu akiwemo Ibrahim Chengula wanakiri wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto kubwa ya wazazi kushinikiza watoto wao kujiferisha mitihani na kuhitaji hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.
"kuna baadhi ya wazazi wanasababisha watoto wao kuto kufika shuleni kwa kuona hakuna haja ya elimu lakini upande mwingine wazazi wanahimiza watoto kushinda nyumbani ili wakasaidie shughuli za shambani"alisema Chengula
Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe ni miongoni mwa halmashauri mbili za mwisho kitaaluma kati ya 6 za mkoa wa Njombe 2019.
from MUUNGWANA BLOG
Comments
Post a Comment