Jinsi ya kupika futari ya Vibibi vya Tui la Nazi


Vipimo
Mchele 2 Vikombe
1. Tui la nazi zito 2 Vikombe
2. Hamira 1 Kijiko Cha chai
3. Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu
4. Iliki Kiasi upendavyo
5. Sukari Kiasi upendavyo
6. Yai 1.

Vipimo vya Tui la Kupaka
1. Tui la nazi 2 Vikombe
2. Hiliki ya unga Kiasi upendacho
3. Sukari Kiasi upendacho
4. Unga wa ngano 1 Kijiko cha supu.

Namna ya Kutayarisha na Kupika
• Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo.

• Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito.

• Osha na loweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.

• Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.

• Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya.

• Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure/uvimbe
Ukishafura, weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo)
Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote.
Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au samli kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko ukitumia upawa na ufunike.

Kibibi kikianza kuiva na kushikana upande mmoja , kigeuze upande wa pili mpaka kigeuke rangi na kuiva.

Panga kwenye sahani iliyopakwa tui.
Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; kila ukiepua kibibi, panga juu ya mwenzake.

from MUUNGWANA BLOG

Comments

Popular posts from this blog