Wakenya washangazwa na Vazi la Waziri Mkuu wa Fiji


Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi.

Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.

Vazi alilovalia ni maarufu nchini Fiji kwa wanaume wa likifahamika kama na jina Suti ya Sulu.

Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.

Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra, Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino.

Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kutumia pini.

Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji Tangu enzi za ukoloni katika katika karne ya kumi na tisa. Mwanzo zililetwa na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizi zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na ukristo.

Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.

Sulu za wanaume wanazovaa rasmi huitwa -sulu vakataga, Sulu zilizoshonwa na mifuko huvaliwa kawaida kama vazi la ofisi na rasmi pamoja na shati na viatu vya wazi (sandozi) na upande wa juu huvaa koti na tai.

Katika hali fulani, mtu anapoingia na Sulu kanisani huonekana kama mtu mwenye heshima nchini Fiji, Sulu zilizoshonwa pia huvaliwa kama sare za polisi na jeshi.

Vazi rasmi la sulu huwa na urefu hadi chini ya magoti na hukatwa kwa mathalani umbo la pembe tatu.

Huku uvaaji wa Sulu mara nyingi huwa ni wa lazima kwa Wafiji wakati fulani, baadhi ya jamii wakati mwingine hukatazwa kuzivaa.



from MUUNGWANA BLOG

Comments

Popular posts from this blog