Ashikiliwa na TAKUKURU kwa kumpa rushwa Mwanasheria wa CCM


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia watu watatu akiwamo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa ambaye anatuhumiwa kutoa rushwa ya Sh 200,000 kwa Wakili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Goodlucky Mwangomango, ili ampe upendeleo kwenye kikao cha kujadili mikataba ya miradi ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema, tukio hilo limetokea Mei 29, mwaka huu, saa nne asubuhi, maeneo ya Sea View Upanga kwenye mgahawa wa Central Park.

Amesema Chandulal ambaye ni mpangaji wa  maeneo ya biashara ya CCM alitoa kiasi hicho ili apewe upendeleo kwenye kikao cha chama hicho cha kufanya marejeo ya mikataba.

“Mtuhumiwa Chandulal atafikishwa mahakamani chini ya kifungu Cha 15 (1), (b) cha Sheria ya Takukuru Na.11/2007,” amesema Myava.

Myava alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

from MUUNGWANA BLOG

Comments

Popular posts from this blog