Miaka mitatu baada ya Ferguson:Manchester united
Soka sasa limebadilika Mno. Kimsingi ladha halisi ya mpira wa miguu inapotea kwa kiasi kikubwa mno. Kuanzia kwa makocha wenyewe, wamiliki wa vilabu hivi, wachezaji mpaka mashabiki hali inayopelekea kupunguza ladha halisi ya mpira wenyewe. Wamiliki pamoja na mashabiki wa vilabu hivi hasa vilabu vikubwa, kwa kiasi kikubwa mara nyingi huwa wanakosa sana uvumilivu wa timu zao kutofanya vizuri. Wanalazimisha mabadiliko ya ghafla ambayo kamwe hayawezekani kwa mchezo wa soka. Kutokana na hali hiyo, makocha wengi wa siku hizi wanajikuta wakifundisha soka la kupata matokeo tu na sio soka hasa la kuburudisha linaloambata na matokeo. Muda wanaopewa kufundisha timu hizi ni mdogo mno kutokana na kukosekana kwa uvumilivu kwa wamiliki na mashabiki. Na hivyo kusababisha ladha halisi ya mchezo wa soka kupungua, na ili kuendana na hali hii ndiyo maana unakuta siku hizi kuna wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ila pasipo kucheza nafasi hizo kwa ufanisi wa hali ya juu kut...