Cheka amlilia Mashali, kumbe pambano lao lilikuwa limekaribia

Bondia mahiri nchini, Francis Cheka ameonyesha hisia zake kutokana na kifo cha bondia mwingine, Thomas Mashali.

Mashali ameuwawa na watu wasiojulikana, inadaiwa mwili wake umetupwa katika eneo la Kimara jiji Dar es Salaam.

Kupitia mtandao wa facebook, Cheka ameandika akionyesha masikitiko yake kwa Mashali ambaye walipokutana mara ya mwisho, Mashali alimshinda Cheka na kuwa bondia namba moja nchini, kwani pia alikuwa amewahi kumshinda Dulla Mbabe ambaye sasa anatamba.

Cheka ameandika: “Ilikuwa ni heshima kuingia ulingo mmoja na wewe ndugu yangu Thomas Mashali, tulipanga tukutane tena 26/11, kweli hakuna aijuae kesho, oila Mungu.

“Ulale mahali pema peponi ndugu yangu, Mungu akutangulie.”

Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog