Bondia Thomas Mashali afariki

Dar es Salaam. Bondia Thomas Mashali (pichani) amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana Kimara, Dar es Salaam.
Mwili wa Bondia huyo umeifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili huku taratibu za mazishi zikiendelea nyumbani kwake Kwa Mtogole, Dar es Salaam.
Mmoja wa wanafamilia wa Bondia huyo, ambaye hakutaka kuandikwa alilithibitishia Mwananchi kutokea kwa kifo cha Bondia huyo.
Mapema jana, Mashali alishiriki kwenye kongamano la ngumi na kuchangia mada ya mabondia kunyanyaswa na mapromota kwenye mapambano.

Comments

Popular posts from this blog