Sukari ya Mtibwa yakolea Msimbazi



Pengine ni matokeo ya usajili bora uliofanywa na klabu ya Simba msimu huu ndiyo umekuwa siri ya mafanikio ya klabu hiyo, hasa baada ya wachezaji watano wapya kutengeneza rekodi ya kuvutia kuliko ilivyokuwa misimu iliyopita.

Kwanza, nyota wapya watatu waliosajiliwa na Simba wakitokea Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim na Muzamiru Yassin wameonekana kuwa mhimili mkubwa kwa timu hiyo msimu huu baada ya kutengeneza safu imara ya ushambuliaji iliyofunga mabao 24 hadi sasa, 14 kati ya hayo yakitoka kwa watoto hao wa Mtibwa.

Ibrahim na Kichuya walitua Simba wakiwa wachezaji wa kawaida, lakini wameibeba timu kwa kuifungia mabao 10 msimu huu, huku Muzamiru akiongeza mengine manne na kuifanya timu hiyo kuwa na wachezaji wengi ambao wenye uwezo wa kufumania nyavu, tofauti na msimu uliopita ilipomtegemea zaidi Mganda Hamis Kiiza.

Simba iliyoifunga Mwadui FC mabao 3-0 juzi na kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ikiwa na pointi 32 kwa mabao ya Ibrahim mawili na Kichuya aliyefunga  moja. Hata hivyo, takwimu za utendaji wa wachezaji hao zinaonyesha kuwa kati ya mabao 24 ya Simba msimu huu, mabao 21 yamefungwa na wachezaji wapya, jambo linalothibitisha kuwa usajili  mzuri uliofanywa na klabu hiyo ya Msimbazi na mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumnasa kocha Joseph Omog, raia wa Cameroon yamezaa matunda.

Comments

Popular posts from this blog