Wakesha siku 3 chini ya mti kupinga ujenzi wa kiwanja cha ndege

Zaidi ya watu miambili wa  jamii ya kifugaji kutoka kabila ya Watatoga  katika kijiji cha Vilima vitatu  wilaya ya Babati wamelalamika kukesha chini  ya miti kwa zaidi ya siku tatu kupinga hatua ya mwekezaji kutaka kujenga uwanja wa Ndege kwenye eneo wanalodai kuwa ni la mapito na malisho ya wanyamapori pamoja na mifugo yao bila kuwashirikisha wananchi.

ITV ilifika kwenye kijiji cha Vilima vitatu na kushuhudia kundi kubwa la watu hao wakiwa chini ya miti  karibu na eneo ilo na wengine wakiandamana kupinga ujenzi huo wa uwanja wa Ndege kinyume na taratibu  kisha wakaeleza kilichowasibu hadi kufikia maamuzi hayo na wanawake nao wakalalamikia vitendo vya unyanyaswaji wanavyofanyiwa. 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji nchini Kusundwa Wamalwa amesema matatizo mengi ya wafugaji yamekuwa yakisababishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji  wanaotumia kutojuwa kwa wafugaji kujinufaisha binafsi.

ITV ilimtafuta mwekezaji anayelalamikiwa  Nicolaus Neglig ili kupata ukweli wa malamiko hayo ambaye alionesha kushangaa na kudai kuwa yeye hana matatizo yoyote na wananchi na kila analolifanya limebarikiwa na serikali ya kijiji cha Vilima vitatu.

Comments

Popular posts from this blog