Miaka mitatu baada ya Ferguson:Manchester united
Soka sasa limebadilika Mno. Kimsingi ladha halisi ya mpira wa miguu inapotea kwa kiasi kikubwa mno.
Kuanzia kwa makocha wenyewe, wamiliki wa vilabu hivi, wachezaji mpaka mashabiki hali inayopelekea kupunguza ladha halisi ya mpira wenyewe.
Wamiliki pamoja na mashabiki wa vilabu hivi hasa vilabu vikubwa, kwa kiasi kikubwa mara nyingi huwa wanakosa sana uvumilivu wa timu zao kutofanya vizuri. Wanalazimisha mabadiliko ya ghafla ambayo kamwe hayawezekani kwa mchezo wa soka.
Kutokana na hali hiyo, makocha wengi wa siku hizi wanajikuta wakifundisha soka la kupata matokeo tu na sio soka hasa la kuburudisha linaloambata na matokeo. Muda wanaopewa kufundisha timu hizi ni mdogo mno kutokana na kukosekana kwa uvumilivu kwa wamiliki na mashabiki.
Na hivyo kusababisha ladha halisi ya mchezo wa soka kupungua, na ili kuendana na hali hii ndiyo maana unakuta siku hizi kuna wachezaji wengi wanaoweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ila pasipo kucheza nafasi hizo kwa ufanisi wa hali ya juu kutokana na kucheza kwenye viwango vya kawaida sana.
Tuangalie Man United na mabadiliko yake kwa miaka hii mitatu tangu Sir Alex Ferguson aondoke kwenye timu ile.
Mpaka Sasa Man United imekua na makocha watatu kwa muda huu mfupi tangu Ferguson aondoke.
Na hawa makocha wamekua na filosofia tofauti tofauti za ufundishaji na kusababisha timu hiyo isiweze kurudi kwenye ubora wake.
Ferguson mwenyewe alikua anafundisha soka aina ya ‘direct football’, mfumo halisi wa soka la kiingereza na ndiyo maana Man United imekua bora kwa mfumo huo kwa miaka mingi sana.
Baada ya Ferguson kuondoka akaja David Moyes ambae pia anafundisha soka la aina hiyo licha ya ukweli kuwa hakuwa mtu sahihi wa kuifundisha United. Kwa dunia ya sasa ile timu ilikua kubwa mno kuliko kocha mwenyewe haikuwa rahisi kumudu mahitaji ya timu ile.
Baada ya Moyes kuondoka Man United wamlileta Lous van Gaal ambaye alikua ana filosofia za tofauti mno na makocha waliomtangulia. Huyu hakuwa muumini wa direct football kabisa.
Hapa ndipo hii timu ikaanza kuyumba zaidi. Louis van Gaal ana personality ya kuweza kumudu sana kuwa kocha wa Man United bila tatizo, ila naye akakumbwa na tatizo lile lile alilokutana nalo Moyes kutokuwepo na uvumilivu na kumpa muda wa yeye kujenga timu yake vile anavyoona ni sahihi.
Ukiangalia Van Gaal hakutaka kufanya kazi ya kupata tu matokeo kimkato mkato kama mashabiki walivyokua wanataka, bali alikua anaisuka timu kuanzia kwenye kiini ili timu ikianza kufanikiwa iwe na mafanikio ya muda mrefu.
Kwa kiasi fulani Van Gaal ana asili fulani kama aliyo nayo Arsene Wenger ya kujenga timu kwa muda mrefu ili iwe na mafanikio ya muda mrefu wachezaji waweze kukaa vizuri kwenye mfumo.
Naye hakukaa muda mrefu sana akafukuzwa akaja Mourinho. Ukiangalia kati ya Van Gaal na Mourinho wana utofauti mkubwa mno kwenye filosofia za ufundishaji.
Van Gaal ni kocha ambaye ana amini kwenye soka la kuvutia na kusuka timu kuanzia kwenye kiini.
Mourinho ni kocha anayehitaji matokeo zaidi kuliko kujali soka linavyochezwa na timu yake sio muumini sana wa soka la pasi nyingi.
Ila hata Mourinho naYe anakutana na presha ileile mashabiki kuhitaji matokeo zaidi ya hali halisi ilivyo.
Ukiangalia kwa miaka hii mitatu hii timu ya Man United imekua haina muendelezo mzuri kati ya kocha awali na kocha anayefuatia.
Kumekua na kuanzishwa kwa style mpya ya uchezaji pale kila kocha mpya anavyokuja hali ambayo inasababisha wachezaji kuanza upya kuuelewa mfumo kila msimu hali hii kimsingi huathiri sana timu.
Na bahati mbaya mashabiki hawana uvumilivu kabisa kwenye soka la sasa wanataka matokeo kirahisi mno bila kuelewa ugumu wa kazi ya kujenga timu.
Jose Mourinho Ni kocha mzuri sana hasa kwenye ufundishaji wa soka la kisasa. Ila kimsingi ukimfatilia hata huko nyuma hua anafanya vizuri zaidi kwenge msimu wake wa pili akiwa na timu husika.
Kwa hiyo Man United inahitaji impatie nafasi ya kutosha kocha huyu aweze kuirudisha timu kwenye ubora wake halisi. Kwa sasa anachofanya Mourinho ni kujaribu kupata matokeo wakati huo huo akijaribu kuingizA mifumo yake na kuondokana ile ya Van Gaal ambayo ni tofauti kabisa na namna yake ya ufundishaji.
Mashabiki wanapaswa wawe na uvumilivu sana kwe kipindi hiki cha mpito. Mpira wa miguu sio mchezo rahisi kama wanavyodhani .

Comments
Post a Comment