KLAUS Kindoki leo amekuwa shujaa wa Yanga baada ya kuokoa penalti ya mwisho iliyopigwa na nahodha wa timu ya Alliance FC, Siraj Juma. Dakika 90 za mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali ulikamilika kwa Alliance kutoshana nguvu na Yanga kwa kufungana bao 1-1. Yanga walitangulia kufunga bao dakika ya 38 lililofungwa na Heritier Makambo na kwa upande wa Alliance bao lilifungwa na Johson James. Baada ya mwamuzi kuamua matuta, Yanga walianza kupiga kupitia beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aligongesha kwenye mwamba, Paul Godfery alifunga penalti yake,Thaban Kamusoko alifunga kwa staili ya paneka, Mrisho Ngassa penalti yake iligonga mwamba na Haruna Moshi alifunga penalti kiufundi. Kwa upande wa Alliance penalti ya kwanza ilifungwa na Joseph John, Martin Kigi aligongesha kwenye mwamba, Dickson Ambundo alikosa penalti yake, Jofrey Luseke alifunga penalti na Samir Vincent alifunga. Baada ya kumaliza penalti 5 za awali kwa timu zote matokeo yalisoma 3-3 baada ya Yanga kukosa penalti ...