ALLIANCE: TUNATAKA TUIFUNGE YANGA YENYEWE YA MWINYI ZAHERA NA MAKAMBO

UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa wapinzani wao Yanga leo wajipange kupokea kichapo kwani kikosi kimejipanga kiasi cha kutosha kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema gharama ya kambi nchini Rwanda leo lazima ijibu na walifanya hivyo makusudi ili kuzoea mazingira ya kupannda ndege na hali ya hewa nje ya Taifa la Tanzania.

"Ujue kikosi kiliweka kambi nchini Rwanda ni mkakati makini kwa wachezaji kuanza kuelewa namna hali ya hewa nje ya nchi ilivyo kabla ya kubeba kombe na kuiwakilisha nchi kimataifa hivyo kuna kitu kimekaa kwenye vichwa vya wachezaji kwa sasa.

"Mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindaini ila kazi yetu leo iakuwa ni kusambaza upendo na misumari ya moto kwa wapinzani wetu, tumewekeza kiasi cha kutosha na tunataka tuifunge Yanga yenyewe ya Heritier Makambo na Mwinyi Zahera," amesema Mwafulango.

 Timu itakayopenya leo hatua ya robo fainali itakutana na Lipuli FC ambayo inamsubiri mshindi wa leo.


from SALEH JEMBE

Comments

Popular posts from this blog