MATOLA AMTISHA MWINYI ZAHERA


Kocha Msaidizi wa Lipuli FC, Suleiman Matola, amesema kuwa mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Yanga utakuwa wa aina yake.

Matola ameeleza kuwa mechi hiyo itakuwa na changamoto kubwa ambapo hata wao wanahitaji ushindi ili kutinga hatua ya fainali.

Yanga imeingia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Alliance Schools kwa mabao 4-3 yaliyopatika kwa njia ya penati baada ya dakika 90 kwenda 1-1.

Baada ya Yanga kuungana na Lipuli, Matola amesema hata Yanga wakija na Kocha wao Mwinyi Zahera haitakuwa sababu ya wao kushindwa kupata matokeo.

"Tunajua Zahera hakuwepo wakati Yanga tunaifunga bao 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu.

"Sasa hata kama akija hakuna sababu ya kutomfunga, ni jambo la kawaida.

"Tunaendelea na maandalizi ili kuja kuhakikisha tunatinga fainali." amesema Matola.

from SALEH JEMBE

Comments

Popular posts from this blog