POGBA ATENGEWA BILIONI 381 MADRID


REAL Madrid inataka kuanza mikakati rasmi ya kumsajili staa wa Manchester United, Paul Pogba mwishoni mwa msimu huu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Pogba mwenyewe ambaye ana umri wa miaka 26 kufunguka kuwa ana ndoto ya kuichezea timu hiyo siku moja.

Pogba alikiri hivyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika majukumu ya kuichezea timu yake taifa ya Ufaransa, kauli hiyo imedaiwa kuiamsha Madrid katika mpango wa kukamilisha dili.

Pogba alieleza kuwa anatakani siku moja afanye kazi na Zinedine Zidane ambaye ni kocha wa sasa wa Madrid.

Imefahamika kuwa Real Madrid imetenga pauni milioni 125 (Sh bilioni 381) kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo. Ikumbukwe kuwa Pogba aliitosa Real Madrid na kuamua kusajiliwa na Manchester United kwa pauni milioni 89, miaka miwili iliyopita.

Madrid wanajua kuwa Mfaransa huyo ana furaha kwenye timu yake ya sasa lakini hana mpango wa kumalizia maisha yake ya soka akiwa klabuni hapo.

“Tunajua Paul ana mkataba na Madrid wanamuwania. Zidane alikuwa mmoja wa waliomshawishi kipindi kile arejee United lakini sasa anaweza kumshawishi ajiunge naye Madrid,” kilisema chanzo cha habari kutoka Man United.

from SALEH JEMBE

Comments

Popular posts from this blog