Posts

Showing posts from October, 2017

MATOLA KUCHOMOA MMOJA SIMBA, YANGA AU AZAM FC

Image
Kocha Mkuu wa Lipuli Fc ya Mkoani Iringa, Selemani Matola ameweka wazi mpango wake wa kuomba mshambuliaji wa mkopo kutoka kwa timu kubwa hapa nchini za Simba, Yanga na Azam ili kuimarisha eneo lake la ushambuliaji katika timu yake ya Lipuli Fc. Matola alisema kwa sasa timu yake inafanya vizuri lakini bado haijafikia malengo aliyojiwekea huku changamoto kubwa ikiwa katika eneo la ufungaji. "Nimepanga kuomba wachezaji ambao hawana nafasi kwenye hizi timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, kuna wachezaji wazuri wanaoweza kutusaidia," alisema Matola ambaye ni mchezaji wa zamani na kocha msaidizi wa Simba. "Eneo la ushambuliaji ndiyo changamoto kubwa kwetu, kama tutaliweka sawa basi timu itakwenda vizuri, nimepanga kupeleka maombi mapema kwani dirisha dogo limekaribia," alimaliza Matola USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Youtube Chanel Down...

TAZAMA HAPA LIVE MECHI ZOTE ZA UCL IFIKAPO SAA 22:45

Image
BOFYA HAPA KUTAZAMA MECHI LIVE OLYMPIACOS VS BARCELONA SAA 22:45 BOFYA HAPA KUTAZAMA MECHI LIVE MANCHESTER UNITED VS BENFICA SAA 22:45 BOFYA KUTAZAMA MECHI LIVE AS ROMA VS CHELSEA SAA 22:45 BOFYA HAPA KUTAZAMA MECHI LIVE CELTIC VS BAYERN MUNICH SAA 22:45 BOFYA HAPA MECHI LIVE PSG VS ANDERLECHT SAA 22:45 BOFYA HAPA KUTAZAMA MECHI LIVE SPORTING LISBON-VS-JUVENTUS. SAA 22:45 USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Youtube Chanel Download Nijuzehabari Blog Android Application On Play Store  Click There WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

SIMBA YAKANUSHA UVUMI UNAOENEZWA KUHUSU KOCHA JOSEPH OMOG

Image
Baada ya kuwepo kwa habari zisizo rasmi kuwa Klabu ya Simba imeachana na Kocha wake Mkuu Mcameroon Joseph Omog Simba wameibuka na kukanusha vikali taarifa hizo. Uongozi wa Klabu ya Simba unakanusha vikali uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu pamoja na vyombo vya habari kuwa umeachana na Kocha Mkuu Joseph Omog.  Uongozi wa Simba unakanusha habari hiyo na kuendelea kusisitiza kuwa Kocha Omog ndio kocha Mkuu na hakuna mabadiliko yoyote kwenye benchi la ufundi la kikosi cha Simba.  'Habari zetu zote rasmi tunazitoa kwenye njia zetu rasmi za habari, kwenye Simba App au mitandao yetu rasmi ya kijamii, watu wapuuzie habari hizi ambazo watu wamekuwa wakizipika kwa maslahi yao binafsi' Alisema Kaimu Makamu wa Rais  Idd Kajuna kuhusiana na tangazo linalosambazwa na watu wasioitakia mema klabu ya Simba Sc. USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Yout...

KILICHOJILI KWENYE MKUTANO WA SIMBA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Image
Afisa Habari wa Klabu ya Simba katika mkutano wake na wandishi wa habari alikuwa na Ajenda 3 ambao ameziweka wazi kwa watanzania na wapenzi wa soka wote. Manara ameweka wazi suala la maandalizi ya Simba kuelekea mechi inayofuata dhidi ya Mbeya City na kusema timu ilianza mazoezi jana katika kujiandaa na mechezo huo utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Sokoine. Kuhusu majeruhi Manara amesema majeruhi ni wale wale mpaka sasa klabu haina ongezeko la majeruhi, wachezaji wote ambao si majeruhi wako vizuri kwa ajili ya mchezo huo. Wachezaji wa Simba ambao ni majeruhi mpaka sasa ni Shomary Kapombe, Said Mohamed "Nduda" na Salim Mbonde. Kuhusu safari ya kuifuata Mbeya City, Manara amesema klabu itaondoka Ijumaa kama Mungu akijalia kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili November 05-2017 na baada ya hapo klabu itacheza mchezo wa kirafiki lakini bado haijajulikana ni timu gani. Manara katika mkutano huo ameonyesha kuwashangaa  wachambuzi wa mpira wa Ta...

MKATABA WA SHIZA KICHUYA USIPIME MWANANGU

Image
KITENDO cha winga wa Simba, Shiza Kichuya kuendelea kutamba hasa anapokutana na Yanga, kimeiweka Simba kwenye wakati mgumu kuzungumza naye kuhusu mkataba mpya. Kichuya aliyejiunga na Simba mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar kwa ada ya usajili ya kawaida, amekuwa moto klabuni hapo na kuiweka timu hiyo katika hali ngumu wakati huu akielekea mwishoni mwa mkataba wake. Kichuya alisaini Simba miaka miwili na huu ndiyo msimu wa mwisho klabuni hapo. Simba ilifanya usajili mkubwa msimu huu kuwashusha nyota wa maana wakiwemo Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima waliogharimu zaidi ya Sh 150 milioni, lakini Kichuya ameendelea kuwa staa mkubwa zaidi klabuni hapo jambo ambalo linawafanya kuanza kujipanga kumpatia mkataba mnono. Tangu amejiunga na Simba mwaka jana, Kichuya ameifungia timu hiyo mabao 16 Ligi Kuu na moja katika kombe la FA hivyo kuwa mchezaji aliyefunga zaidi klabuni hapo katika kipindi cha miezi 14 iliyopita. Katibu Mkuu wa Simba, Dk.Anord Kashembe alisema; "Siwezi kusema k...

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE OCTOBER 31-2017

Image
Chelsea wako tayari kumpa mkataba mpya kiungo wa kati Cesc Fabregas baada ya kummezea mate mchezaji huyo wa umri wa miaka 30 wa Manchester United. (Times) Arsenal wana mpango ya kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Napoli Jorginho 25. (Tuttomercato, via Star) Everton wanamtaka meneja wa Burnley Sean Dye kuwa meneja wao mpya na huenda wakawasiliana naye katika kipindi cha saa 24 zinazokuja. (Sky Sports) Wing'a wa Leicester Riyad Mahrez, 26, analengwa na Marseille. (Mundo Deportivo - in Spanish) Klabu ya Shanghai Shenhua kinamtaka mshambuliajia wa Brighton na Israel Tomer Hemed, 30. (Sun) Hatma ya Slaven Bilic katika klabu ya West Ham bado haijulikani. (Mirror) Mchezaji wa safu ya kati wa Roma na Ubelgiji Radja Nainggolan, 29, anasema kuwa hakuwa na fikra za kuhamia Chelsea msimu uliopita. (Sky Sports) Mfanyabiashara kutoka Dubai Amanda Staveley anaweza kiununua klabu ya Newcastle United. (Newcastle Chronicle) Mshambuljia Tammy Abraham, ambaye yuko Swansea kwa mkop...

RATIBA YA YANGA SC: MECHI 7 ZINAZOKAMILISHA AWAMU YA KWANZA (VPL) 2017-2018

Image
Nijuzehabari.com inakuletea mechi 7 za Yanga Sc zilizobaki ili kukamilisha Awamu ya kwanza ya Ligi Kuu katika kuwania Ubingwa msimu wa 2017-2018. Ratiba mechi za Yanga Sc zilizobaki Mzunguko wa kwanza ziko hivi baada ya kumaliza mchezo wake na Simba, huku timu hizo zikitoa sare ya goli 1-1. Yanga imebakiza mechi 7 tu kukamilisha mzunguko wa kwanza kabla ya kuanza mzunguko wa pili hapo January 2019. November 04-2017 Singida United itaikaribisha Yanga Sc katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. November 12-2017 Yanga itaikaribisha Mbeya City November 18-2017 Yanga Sc itaikaribisha Tanzania Prisons November 25-2017 Mbao Fc itaikatibisha vs Yanga Sc December 02-2017 Yanga itaikaribisha Mwadui Fc December 24 -2017 Yanga itaikaribisha Ruvu Shooting Mechi ya mwisho itakuwa December 30-2017 Yanga itaikaribisha Azam Fc Hapo timu zitaingia mapumziko ya siku 18 ili kujiandaa kwa awamu  ya pili. Ligi hiyo itaendelea tena tarehe 19 January 2018 huku Yanga ikianza na Lipuli Fc, ...

RATIBA YA SIMBA SC: MECHI 7 ZINAZOKAMILISHA AWAMU YA KWANZA (VPL) 2017-2018

Image
Nijuzehabari.com inakuletea mechi 7 za Simba Sc zilizobaki ili kukamilisha Awamu ya kwanza ya Ligi Kuu katika kuwania Ubingwa msimu wa 2017-2018. Ratiba mechi za Simba zilizobaki Mzunguko wa kwanza ziko hivi baada ya kumaliza mchezo wake na Yanga, huku timu hizo zikitoa sare ya goli 1-1. Simba imebakiza mechi 7 tu kukamilisha mzunguko wa kwanza kabla ya kuanz mzunguko wa pili hapo January 2019. November 05-2017 Mbeya City itaikaribisha  Simba Sc Sokoine- Mbeya November 11-2017 Tanzania Prisons itaikaribisha Simba Sc November 19-2017 Simba itaikaribisha Lipuli Fc November 26-2017 Ndanda Fc itaikaribisha Simba Sc December 12-2017 Simba Sc itaikaribisha Singida United December 23-2017 Simba itaikaribisha  Kagera Sugar Mechi ya mwisho itakuwa December 31-2017 Simba ikiikaribisha Majimaji. Hapo timu zitaingia mapumziko ya siku 18 ili kujiandaa kwa awamu  ya pili. Ligi hiyo itaendelea tena tarehe 19 January 2018 huku Simba ikianza na Ruvu Shooting, Simb...

RATIBA YA SOKA: LIGI KUU TANZANIA BARA MZUNGUKO WA TISA (9)

Image
Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea tena wiki hii katika mzunguko wa tisa (9) muendelezo wa Ligi Kuu msimu wa 2017-2018. Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa (8) tunazitazama timu 4 kubwa zote zikiwa zinalinganisha pointi 16 kwa 16 huku zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa Ligi hiyo itaendelea Ijumaa tarehe 03 November 2017 ikizikutanisha Majimaji Fc itakayoiharika Stand United majira ya saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Majimaji- Ruvuma. Baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ijumaa Ligi hiyo  itaendelea tena Jumamosi tarehe 04 November 2017 kwa kuzikutanisha Kagera Sugar itakayoikaribisha Tanzania Prisons saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Kaitaba-Kagera. Ndanda Fc itaikaribisha Mtibwa Sugar saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Nangwanda- Mtwara. Njombe Mji Fc itaikaribisha Mbao Fc saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Sabasaba-Njombe. Singida United itaikaribisha Yound Africans saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma-Dodoma. Azam Fc itaikaribisha Ruvu Sh...

YASOME HAPA MAGAZETI YOTE YA MICHEZO YA LEO JUMANNE OCTOBER 31-2017

Image
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Youtube Chanel Download Nijuzehabari Blog Android Application On Play Store  Click Here WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

RATIBA YA SOKA: MICHUANO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE OCTOBER 31-2017

Image
Michuano ya UCL, Uefa Champions League itaendelea leo Jumanne kwa hatua ya makundi. Hapa nimekuwekea ratiba na muda kamili wa kuanza kwa mechi hizo, kumbuka mechi hizi zitakuwa live hapa hapa nijuzehabari.com kuanzia muda huo. Champions League - Group A October 31 22:45 Basel vs CSKA Moscow 22:45 Manchester United vs Benfica Champions League - Group B October 31 22:45 Celtic vs Bayern Munich 22:45 Paris Saint Germain vs Anderlecht Champions League - Group C October 31 22:45 Atletico Madrid vs Qarabag FK 22:45 Roma vs Chelsea Champions League - Group D October 31 22:45 Olympiacos vs Barcelona 22:45 Sporting CP vs Juventusà USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Youtube Chanel Download Nijuzehabari Blog Android Application On Play Store  Click Here WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

HAYA HAPA MAGAZETI YOTE YA LEO JUMANNE OCTOBER 31-2017 & MICHEZO

Image
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii Instagram Facebook  Twitter Subscribe Youtube Chanel Download Nijuzehabari Blog Android Application On Play Store  Click Here WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII