MATOLA KUCHOMOA MMOJA SIMBA, YANGA AU AZAM FC

Kocha Mkuu wa Lipuli Fc ya Mkoani Iringa, Selemani Matola ameweka wazi mpango wake wa kuomba mshambuliaji wa mkopo kutoka kwa timu kubwa hapa nchini za Simba, Yanga na Azam ili kuimarisha eneo lake la ushambuliaji katika timu yake ya Lipuli Fc.

Matola alisema kwa sasa timu yake inafanya vizuri lakini bado haijafikia malengo aliyojiwekea huku changamoto kubwa ikiwa katika eneo la ufungaji.

"Nimepanga kuomba wachezaji ambao hawana nafasi kwenye hizi timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, kuna wachezaji wazuri wanaoweza kutusaidia," alisema Matola ambaye ni mchezaji wa zamani na kocha msaidizi wa Simba.

"Eneo la ushambuliaji ndiyo changamoto kubwa kwetu, kama tutaliweka sawa basi timu itakwenda vizuri, nimepanga kupeleka maombi mapema kwani dirisha dogo limekaribia," alimaliza Matola
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI
JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii

WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Comments

Popular posts from this blog