KILICHOJILI KWENYE MKUTANO WA SIMBA NA WAANDISHI WA HABARI LEO
Afisa Habari wa Klabu ya Simba katika mkutano wake na wandishi wa habari alikuwa na Ajenda 3 ambao ameziweka wazi kwa watanzania na wapenzi wa soka wote.
Manara ameweka wazi suala la maandalizi ya Simba kuelekea mechi inayofuata dhidi ya Mbeya City na kusema timu ilianza mazoezi jana katika kujiandaa na mechezo huo utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Sokoine.
Kuhusu majeruhi Manara amesema majeruhi ni wale wale mpaka sasa klabu haina ongezeko la majeruhi, wachezaji wote ambao si majeruhi wako vizuri kwa ajili ya mchezo huo.
Wachezaji wa Simba ambao ni majeruhi mpaka sasa ni Shomary Kapombe, Said Mohamed "Nduda" na Salim Mbonde.
Kuhusu safari ya kuifuata Mbeya City, Manara amesema klabu itaondoka Ijumaa kama Mungu akijalia kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili November 05-2017 na baada ya hapo klabu itacheza mchezo wa kirafiki lakini bado haijajulikana ni timu gani.
Manara katika mkutano huo ameonyesha kuwashangaa wachambuzi wa mpira wa Tanzania na kusema nawashangaa wachambuzi wetu wanashindwa kukemea waamuzi mabovu dhidi ya Yanga wao wanazungumzia thamani ya kikosi Simba akimbatanisha kuwa kuna mtu anayejua thamani ya kikosi cha Yanga?.
"Tunadhulumiwa hadharani halafu wachambuzi mnaacha kuongea ukweli mnaishia kusema tu kikosi cha bilioni moja kimeshindwa kuifunga Yanga".
“Sasa leo nimewaletea video muone uonevu tunaofanyiwa, na huu ndio utakuwa utaratibu wangu kuanzia sasa. Tumeandika barua TFF, chama cha waamuzi na kwa waziri mwenye dhamana ya michezo kuelezea tunavyoonewa,” alisema Manara.
Video hizo zinaoonesha kuonewa kwa klabu yake na waamuzi katika mechi yao na Mbao Fc video hizo zinazoonesha matukio mawili jinsi walivyonyiwa penaliti baada ya Jonh Bocco kufanyiwa faulu mbili za wazi.
Pengine inaonesha Penaliti waliyopewa Stand United kuwa Ally Shomary alishika na nyingine ni ya juzi dhidi ya Yanga Sc, ikionesha Papy Tshishimbi na Kelvin Yondan wakishika mpira kwa nyakati tofauti.
Mwisho Manara amesisitiza kuwa Omog bado ni kocha mkuu wa klabu hiyo huku akishikiliana na kocha msaidizi Masoud Djuma.
"Hakuna mabadiliko yoyote sisi tunaendeea na utaratibu wetu,kocha ni omog,sina taarifa yoyote ya mabadiliko" alimaliza Haji Manara.
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI
WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Video inayomwonesha Kelvin Yondan kuwa alishika mpira.
Video inayoonesha kuwa Tshishimbi alishika mpira.
JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii
WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII
Comments
Post a Comment