SIMBA YAKANUSHA UVUMI UNAOENEZWA KUHUSU KOCHA JOSEPH OMOG

Baada ya kuwepo kwa habari zisizo rasmi kuwa Klabu ya Simba imeachana na Kocha wake Mkuu Mcameroon Joseph Omog Simba wameibuka na kukanusha vikali taarifa hizo.

Uongozi wa Klabu ya Simba unakanusha vikali uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu pamoja na vyombo vya habari kuwa umeachana na Kocha Mkuu Joseph Omog. 

Uongozi wa Simba unakanusha habari hiyo na kuendelea kusisitiza kuwa Kocha Omog ndio kocha Mkuu na hakuna mabadiliko yoyote kwenye benchi la ufundi la kikosi cha Simba. 

'Habari zetu zote rasmi tunazitoa kwenye njia zetu rasmi za habari, kwenye Simba App au mitandao yetu rasmi ya kijamii, watu wapuuzie habari hizi ambazo watu wamekuwa wakizipika kwa maslahi yao binafsi' Alisema Kaimu Makamu wa Rais  Idd Kajuna kuhusiana na tangazo linalosambazwa na watu wasioitakia mema klabu ya Simba Sc.
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI
JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii

WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Comments

Popular posts from this blog