TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMANNE OCTOBER 31-2017

Chelsea wako tayari kumpa mkataba mpya kiungo wa kati Cesc Fabregas baada ya kummezea mate mchezaji huyo wa umri wa miaka 30 wa Manchester United. (Times)

Arsenal wana mpango ya kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Napoli Jorginho 25. (Tuttomercato, via Star)

Everton wanamtaka meneja wa Burnley Sean Dye kuwa meneja wao mpya na huenda wakawasiliana naye katika kipindi cha saa 24 zinazokuja. (Sky Sports)

Wing'a wa Leicester Riyad Mahrez, 26, analengwa na Marseille. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Klabu ya Shanghai Shenhua kinamtaka mshambuliajia wa Brighton na Israel Tomer Hemed, 30. (Sun)

Hatma ya Slaven Bilic katika klabu ya West Ham bado haijulikani. (Mirror)

Mchezaji wa safu ya kati wa Roma na Ubelgiji Radja Nainggolan, 29, anasema kuwa hakuwa na fikra za kuhamia Chelsea msimu uliopita. (Sky Sports)

Mfanyabiashara kutoka Dubai Amanda Staveley anaweza kiununua klabu ya Newcastle United. (Newcastle Chronicle)

Mshambuljia Tammy Abraham, ambaye yuko Swansea kwa mkopo anasema anataka kuichezea Uingerea soka ya kimataifa badala ya Nigeria. (Times)

Gary Neville amemfananisha Jose Mourinho na mwanamasumbwi Floyd Mayweather, alipomtetea meneja huyo wa Manchester United. (Sky Sports)

Mshambualjai wa England Jermain Defoe anahofia kukosa kucheza kombe la dunia kutokana na kutojumuishwa katika mechi za Bournemouth. (Mirror)

Klabu ya China ya Meixian Techand imewapa wachezaji wake pauni milioni 3 kila mchezaji kwa kuiwezesha klabu yao kupanda ngazi hadi divisheni ya pili. (Mail)

Paris St-Germain wamemuorodhesha Philippe Coutinho, 25, kuwa nambari moja kati ya wacheza watakaowawinda msimu unaokuja. (TF1 - in French)

Manchester City wanaamini kuwa wanaweza kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Isco, licha ya yeye kuwa na mkataka wa muda mrefu na Real. (Don Balon, via Daily Express)
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI
JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii

WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Comments

Popular posts from this blog