RATIBA YA SOKA: LIGI KUU TANZANIA BARA MZUNGUKO WA TISA (9)

Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea tena wiki hii katika mzunguko wa tisa (9) muendelezo wa Ligi Kuu msimu wa 2017-2018.

Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa (8) tunazitazama timu 4 kubwa zote zikiwa zinalinganisha pointi 16 kwa 16 huku zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa

Ligi hiyo itaendelea Ijumaa tarehe
03 November 2017 ikizikutanisha
Majimaji Fc itakayoiharika Stand United majira ya saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Majimaji- Ruvuma.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa Ijumaa Ligi hiyo  itaendelea tena Jumamosi tarehe 04 November 2017 kwa kuzikutanisha Kagera Sugar itakayoikaribisha Tanzania Prisons saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Kaitaba-Kagera.

Ndanda Fc itaikaribisha Mtibwa Sugar saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Nangwanda- Mtwara.

Njombe Mji Fc itaikaribisha Mbao Fc saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Sabasaba-Njombe.

Singida United itaikaribisha Yound Africans saa 16:00 jioni katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma-Dodoma.

Azam Fc itaikaribisha Ruvu Shooting saa 19:00 usiku katika Uwanja wa Azam Complex-Dar es salaam.

Baada ya kukamilika kwa mechi hizo za Ijumaa na Jumamosi Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili tarehe 05-11-2017 katika kukamilisha mzunguko wa (9)
Lipuli Fc itaikaribisha Mwadui Fc saa 16:00 katika Uwanja Samora-Iringa.

Mbeya City itaikaribisha Simba Sc ambao ndio vinara wa Ligi saa 16:00 jioni katika Sokoine-Mbeya.
USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI

JIUNGE NA NIJUZEHABARI SASA SASA! Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia mitandao hii

WASHIRIKISHE MARAFIKI ZAKO HABARI HII KUPITIA MITANDAO HII

Comments

Popular posts from this blog