Posts

Showing posts from May, 2017

UZI MPYA MANCHESTER CITY MSIMU UJAO

Image
Manchester City wala hawajataka kuchelewa, mapemaa wameamua kuweka hadharani uzi wao mpya wa msimu wa 2017-18. Uzi huo kwa vikosi vyote, yaani timu kubwa ya wanaume na wanawake, vijana na zile za watoto sasa uko hadharani. Uzi waliouanika Man City ni ule wa blue bahari ambao unajulikana kama "Jezi za Nyumbani". KUPATA HABARI ZOTE ZA MICHEZO NA USAJILI KILA SIKU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK BOFYA HAPA

WACHEZAJI 10 SIMBA KUPIGWA CHINI, 10 KUSAJILIWA

Image
Klabu ya Simba imepanga kuwabakiza wachezaji 15 pekee kati ya 25 iliowasajili msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA). Timu hiyo, inataka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) watakayoshiriki mwakani. Wakati wakipanga kusajili na kuwaacha wachezaji hao, tayari baadhi ya nyota muhimu wa Simba wameshaanza kuaga kwenye timu hiyo akiwemo Abdi Banda ambaye mkataba wake umemalizika, wengine ni Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu ambao wanaelezwa kuwa wanaweza kuondoka kwenye timu hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema kuwa bado hawajapokea rasmi ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog lakini tayari Kamati ya Utendaji ilikutana kufanya tathmini ya kikosi chao kwa ajili ya usajili. Hans Poppe alisema  katika kikao hicho wameona wachezaji kumi ambao hawana mchango na kupanga kuwaondoa katika mipango yao ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kimat...

SIMBA YAAMBULIA KIPOGO MECHI YA KIRAFIKI HUKO KATAVI

Image
WASHINDI wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC leo wameshindwa kufurukuta mbele ya wenyeji, Nyundo FC baada ya kuchapwa mabao 2-1 Uwanja wa Katavi mjini Katavi katika mchezo wa kirafiki. Simba iliyokuwa inacheza mchezo huo kukamilisha msimu kabla ya kuvunja kambi na kuwapa wachezaji wake mapumziko, ilikwenda mapumziko ikiwa tayari imekwishachapwa 2-0. Simba iliyokuwa inacheza mchezo huo kukamilisha msimu kabla ya kuvunja kambi na kuwapa wachezaji wake mapumziko, ilikwenda mapumziko ikiwa tayari imekwishachapwa 2-0. Lakini kipindi cha pili, kocha aliyeiongoza timu leo, Nico Kiondo wa timu B alimuingiza Meneja wa timu, Mussa Hassan Mgosi kwenda kuchukua nafasi ya chipukizi wa timu ya vijana, Mohammed Mussa na ndipo hapo Simba ikapata uhai hata kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi. Mgosi aliichachafya ngome ya Nyundo na kufumua shuti kali, ambalo kipa wa Nyundo alitema na kumkuta mshambuliaji Juma Luizio ali...

TETESI: SIMBA KUACHANA NA DANIEL AGYEI HUYU NDIYE MRITHI WAKE

Image
SIMBA inataka kumuacha kipa Mghana, Daniel Agyei ili imsajili kipa wa Azam FC, Aishi Manula. Na hiyo ni kufuatia habari za Aishi kutokubaliana na Azam kuongeza mkataba, baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa mwezi ujao. Uongozi wa Simba SC unaamini ukimpata Aishi hautakuwa na sababu ya kuingia gharama za ziada kwa kuendelea kuwa na kipa wa kigeni, Agyei aliyejiunga na Wekundu hao wa Msimbazi Desemba mwaka jana kutoka Medeama SC ya Ghana. Hata hivyo, wazo hilo linapingwa na baadhi ya viongozi wa Simba, wanaoamini Agyei ni bora zaidi ya Aishi na ndiye anayeIfaa klabu hIyo kwa sasa ikirejea kwenye michuano ya Afrika. Simba ilikata tena tiketi ya kurudi kwenye michuano ya Afrika, baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Jamhuri Dodoma Jumamosi iliyopita. Na kwa ushindi huo, Simba imekata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka...

USAJILI: SINGIDA UNITED INATISHA YAMNASA HUYU KUTOKA TOTO AFRICAN

Image
Hassan Ramadhan Kessy akijaribu kumtoka  beki wa Toto African Salum Abdalah Chuku Klabu ya Singinda United imeendelea kufanya kweli katika ujenzi wa kikosi chake tayari kwa kwa msimu mpya wa ligi kuu bara msimu ujao hii ni baada ya kufanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Toto Africans ya Mwanza,Salumu Chuku. Chuku aliyeng'ara msimu uliopita licha ya Toto Africans kushuka daraja amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo inayonolewa na Mholanzi Hans Van Pluijm. Chuku anakuwa mchezaji wa tatu mzawa kujiunga na Singida United.Wengine ni Kenny Ally Mwambungu aliyetokea Mbeya City na Atupele Green aliyetokea JKT Ruvu ya Pwani. KUPATA HABARI ZOTE ZA MICHEZO NA USAJILI KILA SIKU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK BOFYA HAPA

LIPULI FC NAYO YAJA KIVINGINE, YATENGA MAMILIONI KWA AJILI YA USAJILI

Image
  Lipuli FC ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja timu nyingine mbili ni Singida United na Njombe Mji Klabu ya Lipuli ya Iringa ambayo itashiriki Ligi ya Vodacom msimu ujao imetenga Sh. Milioni 800, kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi Kuu ya Vodacom Tanzania. Mwenyekiti wa timu hiyo Abduli Majeki, amesema, mbali na kiasi hicho cha fedha pia wapo kwenye mazungumzo na makampuni matatu ili kuwadhamini katika mambo mbalimbali ya kuiimarisha timu yao kwasababu wanataka kufanya vizuri na siyo kushiriki. “Tupo kwenye mazungumzo na makampuni matatu kwa ajili ya kutusaidia kwenye udhamini unajua tuna mkakati wa kununua basi la klabu lakini pia kufanya usajili wawachezaji wenye viwango vya juu ili kuiwezesha timu yetu kufanya vizuri hivyo lazima tuwe na pesa,”amesema Majeki. Kiongozi huyo pia amesema wapo kwenye mazungumzo na kocha Selemani Matola, ili kuweza kuwa kocha wao baada ya kupitia CV zake na kugundua kuwa anavigezo vinavyostaili kuifundi...

HABARI, TETESI ZA USAJILI TANZANIA BARA NA ULAYA MAY 31/2017

Image
Aguero ni moja ya wachezaji bora duniani ,  Tunamhitaji katika kikosi chetu ili kupata mafanikio ( mataji ) .  Aguero Atakuwa nasi katika msimu ujao kwani ni moja ya mchezaji muhimu kwetu "  Hayo ni maneno ya mwenyekiti wa klabu ya manchester City ,  Emirati Al Mubarack  Akithibitisha kwamba sergio Aguero ataendelea kukipiga ndani ya manchester City msimu Ujao .  Kauli hii imekuja muda mfupi baada ya mshambuliaji huyo kuhusishwa kutaka kuihama klabu hiyo huku tetesi zilikuwa zikidai kwamba huenda akatimkia real madrid au manchester United . ESPN  Imemtangaza Christiano ronaldo kuwa ndiye mwanamichezo maarufu zaidi duniani kuliko mwanamichezo yeyote .  Katika listi hiyo Mcheza basketball ,  Lebron James anashika nafasi ya  2 huku Lionel messi akiwa nafasi ya 3 . " Ni kweli nimemwambia kwamba ,  Hii ni nafasi muhimu kwake Kucheza katika timu kubwa Kwani endapo atahitaji Kujifananisha yeye na walio bora ni lazima aen...

DONDOO ZA MICHEZO TANZANIA NA NJE YA TANZANIA MAY 31/2017

Image
Nahodha wa zamani wa  Liverpool Steven gerrad Jana ametimiza miaka 37  Hivi hapa vikombe alivyotwaa katika maisha yake ya soka FA cup vikombe 2 FA Community shield 1 Champion league 1 Uefa Cup 1 Uefa Super Cup 1 Imeripotiwa kuwa Mtendaji mkuu wa klabu ya azam fc Saad  kawemba  Huenda atakua kafukuzwa kazi  azam fc  japo kuwa taarifa hii bado haijathibitishwa. Mwili wa  Marehemu Dada Shose  Fidelis Unatarajiwa kuagwa Hapo kesho Jijini Dar  es laam na utasafirishwa kuelekea moshi kwa ajili ya maziko klabu Ya simba kucheza mchezo wa  kurafiki mkoani katavi hii ikiwa ni  katika zoezi la  kutembeza kombe Lao la #azamSportsFederationCup Mkuu wa mkoa wa  Mwanza Awapongeza mbao fc kwa kucheza Fainali kombe la  shirikisho la  azam sports federation cup Yanga ipo mbioni kunasa Sain Ya Nyota Hawa Mbaraka Yusuph Kagera Sugar Kelvin Sabato  Maji Maji Rafael Daud Mbeya City Salmin Hoza Mbao A...

Tanzia: aliyekuwa Mbunge wa Moshi, Ndesamburo afariki dunia

Image
MBUNGE wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi, Basil Lema, Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe

TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA MAY 31/2017

Image
BEKI wa Mbao FC, Mghana Asante Kwasi, ameipiga chini ofa ya klabu ya Singida United inayofundishwa na kocha Hans van der Pluijm, iliyotaka kumsajili kwa ajili ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, badala yake amesema angependa kujiunga na Azam FC. Akizungumza  jana, Kwasi alisema ana amini Azam FC ni klabu sahihi kwake kujiunga nayo kutokana na kuvutiwa na namna inavyoendeshwa. Alisema kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kumalizika, alifuatwa na wadau wa klabu ya Singida United wakimshawishi ajiunge nao lakini aliwagomea akitaka apewe muda wa kutafakari wapi ni mahali sahihi kwake kutimkia. “Kuna timu nyingi Tanzania lakini navutiwa zaidi na Azam jinsi inavyojiendesha, ni klabu inayofanya mambo yake kisasa sana. “Kuna meneja wangu yupo Afrika Kusini yeye ndio ana jukumu la kunitafutia timu, unajua lengo langu ni kucheza timu itakayonifanya nionekane, hii ndiyo sababu iliyonifanya niipotezee Singida United. Kipa mkongwe wa Yanga, Ally Mustapha 'Ba...

RIYAD MAHREZ KUONDOKA LEICESTER CITY

Image
Kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez amesema kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Le Havre ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa paundi 400,000 mwaka 2014, amesema alikubali kubaki klabuni hapo kwa msimu mwingine baada ya majadiliano mazuri na mwenyekiti walipoishangaza dunia kwa kuwa mabingwa wa EPL msimu uliopita. Lakini kwa sasa amesema kuwa tiyari amekwisha iambia klabu juu ya kuondoka kwake na anaomba wamruhusu kufanya hivyo. Mahrez mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa England mwaka 2016, amecheza mara 48 msimu huu akifunga magoli 10 na kutoa pasi saba za magoli. Leicester ilianza msimu wa ligi ya England vibaya na hatimaye kumaliza katika nafasi ya 12, lakini ikafika hatua ya robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

JOSEPH OMOG KUITUMIA FULSA YA SPORTPESA CUP KUKIJENGA KIKOSI CHAKE

Image
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, amepanga kuitumia michuano ya Kombe la Sportpesa kwa ajili ya kukijenga zaidi kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao. Simba ambayo imemaliza msimu huu ikinyakua Kombe la FA huku ikilikosa Kombe la Ligi Kuu Bara lililotua kwa watani zao wa jadi, Yanga, inatarajiwa kuwa na mapumziko ya takribani siku tano kabla ya kuanza kujiandaa na michuano hiyo. Michuano hiyo itakayozishirikisha timu nane ambazo ni Simba, Yanga, Singida United na Jang’ombe Boys kutoka Tanzania na Tusker, Gor Mahia, Nakuru All Stars na AFC Leopards za Kenya, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 5, mpaka 11, mwaka huu. Omog amesema kuwa: “Tunashukuru tumemaliza msimu salama licha ya kuukosa ubingwa wa ligi kuu, lakini kitendo cha kuchukua Kombe la FA ni faraja kubwa kwetu hali ambayo itatufanya msimu ujao tujipange zaidi. “Baada ya ligi kumalizika, kinafuata kipindi cha usajili ambapo hatutakiwa kufanya makosa kwa hilo na hii michuano midogo ambayo tu...

SHOMARY KAPOMBE AZIJIBU TAARIFA ZA KUEREA MSIMBAZI

Image
BEKI wa Azam FC, Shomary Kapombe amesema kwamba sasa bado hajafikiria kuondoka katika kikosi cha timu yake kutokana na mkataba kumbana. Kuna taarifa kwamba mchezaji huyo huenda akatua Simba kwa msimu ujao, kutokana na sera mpya za usukwaji mpya wa kikosi cha timu hiyo zilizosababisha pia, Nahodha wake John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aondoke. Kapombe amesema kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia suala la kurejea Simba, kwani bado ana mkataba wa muda mrefu na Azam. "Nina mkataba na Azam tena wa muda mrefu, hivyo kama Simba inanihitaji italazimika kwenda kwa viongozi wangu kukaa meza moja," alisema. Shomary Kapombe amesema kwamba hajafikiria kuondoka Azam kutokana na mkataba kumbana Kapombe alitua Azam FC msimu wa 2014 akitokea katika kikosi cha timu ya AS Cannes ya Ufaransa, ambayo nayo ilimchukua kutoka Simba kwa mkopo. Katika hatua nyingine, mdogo wake Shomary, Abbas Kapombe ni kati ya wachezaji watano wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam FC, waliopandishw...

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA TAR 31 MAY 2017 PAMOJA NA YA MICHEZO. Usajili mpya Simba Balaa, Ngoma,Niyonzima wajifunga miaka 2 Msimbazi.Soma zaidi hapa

Image
Habari za asubuhi mdau wangu wa nguvu, leo ni May 31/2017 na kama ilivyo kawaida yangu ya kila siku asubuhi nakuwekea habari kubwa kwenye Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya Hardnews na Michezo ili ujue kinachoendelea pia usiache kukaa karibu nami kila muda kupata Habari zote za Michezo.