USAJILI: SINGIDA UNITED INATISHA YAMNASA HUYU KUTOKA TOTO AFRICAN

Hassan Ramadhan Kessy akijaribu kumtoka  beki wa Toto African Salum Abdalah Chuku

Klabu ya Singinda United imeendelea kufanya kweli katika ujenzi wa kikosi chake tayari kwa kwa msimu mpya wa ligi kuu bara msimu ujao hii ni baada ya kufanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Toto Africans ya Mwanza,Salumu Chuku.
 photo nijuze habari_zpsfbogl9sm.png
Chuku aliyeng'ara msimu uliopita licha ya Toto Africans kushuka daraja amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo inayonolewa na Mholanzi Hans Van Pluijm.

Chuku anakuwa mchezaji wa tatu mzawa kujiunga na Singida United.Wengine ni Kenny Ally Mwambungu aliyetokea Mbeya City na Atupele Green aliyetokea JKT Ruvu ya Pwani.

KUPATA HABARI ZOTE ZA MICHEZO NA USAJILI KILA SIKU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK BOFYA HAPA

Comments

Popular posts from this blog