TETESI ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA MAY 31/2017

BEKI wa Mbao FC, Mghana Asante Kwasi, ameipiga chini ofa ya klabu ya Singida United inayofundishwa na kocha Hans van der Pluijm, iliyotaka kumsajili kwa ajili ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, badala yake amesema angependa kujiunga na Azam FC.

Akizungumza  jana, Kwasi alisema ana amini Azam FC ni klabu sahihi kwake kujiunga nayo kutokana na kuvutiwa na namna inavyoendeshwa.
Alisema kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kumalizika, alifuatwa na wadau wa klabu ya Singida United wakimshawishi ajiunge nao lakini aliwagomea akitaka apewe muda wa kutafakari wapi ni mahali sahihi kwake kutimkia.
“Kuna timu nyingi Tanzania lakini navutiwa zaidi na Azam jinsi inavyojiendesha, ni klabu inayofanya mambo yake kisasa sana.

“Kuna meneja wangu yupo Afrika Kusini yeye ndio ana jukumu la kunitafutia timu, unajua lengo langu ni kucheza timu itakayonifanya nionekane, hii ndiyo sababu iliyonifanya niipotezee Singida United.

Kipa mkongwe wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' na beki wa pembeni wa timu hiyo, Oscar Joshua ni kati ya wachezaji watakaokuwepo kwenye kikosi cha Singida United katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kama hawatakuwa katika kikosi hicho basi safari yao kwa upande wa Yanga itakuwa imeishia hapo.

Barthez na Joshua ni kati ya wachezaji ambao hawakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina katika msimu uliopita wa ligi kuu.

Wachezaji hao wote bado wana mikataba ya mwaka mmoja wa kuichezea Yanga kwenye msimu ujao wa ligi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani wachezaji hao wataondolewa Yanga na kupelekwa Singida inayofundishwa na Kocha Mkuu Mholanzi, Hans Pluijm aliyekuwa anaifundisha timu hiyo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na George Lwandamina.

Mtoa taarifa huyo alisema, wachezaji hao walikuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaochwa katika msimu ujao, lakini kutokana na mikataba yao kutomalizika watapelekwa kwa mkopo.

"Barthez na Joshua hawana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Lwandamina na pia hana mipango nao, hivyo kama uongozi tumeona tuwatoa kwa mkopo.

"Tutawatoa baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Singida na kukubali kuwachukua, hivyo tumeona tuwaachie waende huko wakacheze,"alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Barthez kuzungumzia hilo alisema kuwa ":Bado sijapata taarifa rasmi ya kupelekwa kwa mkopo, ni tetesi ninazozisikia pekee kama ulivyosikia wewe ni vema tukasubiria kwanza kabla ya mimi kuongea chochote.

"Kingine ni ngumu mimi kuondoka kabla ya kupelekwa huko na Yanga, kama unavyojua bado nina mkataba wa kuichezea Yanga,"alosema Barthez.
 photo nijuze habari_zpsfbogl9sm.png

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Juma Mahadhi amesema, hayuko tayari kutolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine, kama itatokea klabu yake inataka kumtoa kwa mkopo ataomba imuache ili akatafute maisha sehemu nyingine.

Hiyo inatokana na tetesi ambazo zimekuwa zikienea kwamba, klabu ya Yanga huenda ikamtoa nyota huyo kwa mkopo kwenda klabu ya Singida United ambayo imepanda kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

“Sipo tayari kutolewa kwa mkopo, kama itatokea hivyo nitaomba waniache niende kutafuta maisha sehemu nyingine. Mimi sijui lolote kuhusu hilo, klabu yangu haijaniambia chochote na kama wataniambia, msimamo wangu ndio huo,” amesema Juma Mahadhi alipozungumza na Sports Extra.

Mahadhi pia amesema alitamani kucheza mechi nyingi katika klabu yake lakini imekuwa tofauti na mipango pamoja na matarajio yake.

“Nilijipanga nicheze mechi nyingi na kuisaidia klabu yangu zaidi ya hapo lakini malengo yangu hayakutimia. Kulikuwa na ushindani mkubwa kwenye kikosi na kila mchezaji aliyepata nafasi alitaka kuonesha anapaswa kucheza kila mechi.”

“Najipanga kwa ajili ya kufanya vizuri katika msimu ujao ili nipate nafasi ya kucheza mechi nyingi tofauti na msimu huu.”

Kuhusu klabu ambazo zinahitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao Mahadhi amesema zipo klabu kadhaa za ndani na nje lakini kwa sasa hawezi kuzitaja kwa sababu bado yupo ndani ya mkataba na Yanga.

“Nimepokea ofa kutoka vilabu mbalimbali ndani na nje ya nchi, kwa sasa siwezi kuzungumzia lolote kwa sababu nipo ndani ya mkataba. Waende wakaonane na manager wangu na viongozi wa klabu wakikubaliana nitafanya maamuzi kwa sababu mpira ni kazi yangu.”

Manula amesema, licha ya timu yake kusajili wachezaji wengi wa kigeni miaka ya hivi karibuni bado Bocco amekuwa mhimili muhimu ndani ya timu yao kutoka na uwezo wake wa kutupia kambani.
“Unapokuwa na mtu kama Bocco katika timu ni kitu kikubwa sana kwa sababu ametoka mbali na Azam na amefanya mengi makubwa, makombe mengi yaliyopatikana ndani ya Azam FC  nadhani ni katika uongozi wake yeye kama nahodha, ni mtu muhimu sana.
“Bocco ni mchezaji ambaye bado alikuwa anahitajika katika klabu ya Azam, kwa sababu unaweza ukaona wachezaji wengi wanaokuja Azam katika nafasi yake hawafanyi vizuri. Wamesajiliwa wachezaji wengi professional waje waisaidie klabu na hawaisaidii mara zote Bocco anakuwa mkombozi na tegemeo.”
“Kitu cha kufikiria ni kwamba, leo Bocco anaondoka nani anakuja? Tunamuona Shabani Idd anakuja vizuri lakini bado ni kijana mdogo anahitaji support kubwa kutoka Bocco kama alivyokuwa anapewa awali. Nilikuwa nawaona wanakaa pamoja na kuzungumza, tukiwa mazoezini anajaribu kumuelewesha kwahiyo walikuwa ni marafiki.”
“Kuondoka kwa Bocco yule kijana anabaki pekeake kusimama mwenyewe itamuwia vigumu. Bocco anaondoka akiwa anategemewa kama top striker na utaona hata wakati yupo nje anasumbuliwa na majeraha timu ilikuwa inayumba.”
“Bocco kaondoka Azam kwa sababu ya maslahi yake hajaondoka kwa sababu Azam wamemchoka au hawahitaji tena kuwa na yeye kwa sababu uwezo wake umeshuka, uwezo wake haujashuka licha ya kusumbuliwa na mejeruhi.”
“Namtakia maisha mema huko anapokwenda na hata tukikutana nadhani hakutakuwa na uadui kwa sababu soka si uadui.”

Juma lililopita afisa habari wa Azam FC Jafar Idd alithibitisha klabu hiyo kuachana rasmi na Bocco baada ya mshambuliaji huyo kudumu kwa muda mrefu ndani ya Azam.

BENCHI la Ufundi la klabu ya Yanga limesema halifahamu kama kiungo wake Deus Kaseke ametimka klabuni humo.

Taarifa za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zinasema kuwa mchezaji huyo yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili kwenye klabu ya Singida United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.

Singida imeanza usajili kwa kasi baada ya kumsajili kocha wa zamani wa Yanga na mkurugenzi wa Ufundi, Hans van der Pluijm na wachezaji watano wa kimataifa, mbali na hao, Singida imehakikishia inaimarisha vyema kikosi chake baada ya kumsajili kiungo mahiri wa Mbeya City, Kenny Ally.

kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema bado wanaamini Kaseke ataendelea kubaki Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Tunachofahamu kuwa Kaseke bado ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuwa katika mipango ya kocha, tunamuamini Kaseke na tunaamini ataendelea kuitumikia Yanga msimu ujao,” alisema Mwambusi.

Kocha huyo wa zamani wa Mbeya City amesema Kaseke bado yupo kwenye mipango ya kocha George Lwandamina kwa ajili ya msimu ujao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Kaseke alisajiliwa na Yanga kipindi cha Pluijm ambaye anatarajia kumsajili ili kuwa naye Singida United kwa ajili ya msimu ujao, mchezaji huyo anaonekana kutamani kwenda Singida United kwa ajili ya kuungana na kocha wake wa zamani.

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe, amewapa mkono wa kwaheri mashabiki wa timu hiyo akisisitiza kamwe hatorudi nchini mpaka atakapolipwa mishahara ya miezi mitatu anayodai.

Tambwe ambaye yupo nchini kwao Burundi kwa ajili ya mapumziko, alisema: “Nipo Burundi, nasikia kuna mashindano huko Dar es Salaam (SportPesa), kurudi huko ni majaliwa sijui lini, wakituwekea mishahara ndio narudi.

“Nasikia wanataka kunipa mkataba wa mwaka mmoja, nipo tayari, lakini nasema hivi, nitarejea huko kwa ajili ya mazungumzo na mambo mengine pindi nitakaposikia wametuwekea mishahara yetu, vinginevyo sirudi.”

Tambwe ni miongoni mwa mastraika waliochezea Yanga kwa mafanikio makubwa tangu alipojiunga na timu hiyo kipindi cha dirisha dogo la msimu wa mwaka 2014/15 akitokea Simba.

Katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi karibuni, Tambwe aliifungia Yanga mabao 11 na kushika nafasi ya nne katika orodha ya wafungaji bora.


Licha ya kubakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake na Yanga, kipa Benedict Tinocco amesema hafikirii kurejea katika timu hiyo ili kulinda kiwango chake.

Tinocco aliichezea Mtibwa Sugar kwa mkopo msimu uliopita licha ya kutakiwa kurudi Yanga, mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Vijana amesema hana mpango huo kwa kuwa hawezi kupata nafasi ya kucheza.

“Ninauthamini sana muda,sidhani kama ninaweza kupata namba, na mimi bado ni kijana mdogo ni kheri nipigane huku kulinda kipaji change kama nitaonekana nitarudi tena kwenye timu yangu.

Msimu uliopita wa Ligi Kuu, Tinocco aliitumikia Mtibwa Sugar na alitoa changamoto kwa kipa Said Mohammed na kufanikiwa kucheza mechi kadhaa za Ligi Kuu ikiwemo ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga ambayo Mtibwa ilifungwa mabao 3-1.

“Nimeitumikia Mtibwa kwa nguvu na nimeshiriki vizuri kila hatua na mechi nilizocheza, nasubiri ripoti ya makocha kama watapendekeza nibaki Mtibwa nitaendelea kuipigania na kama itakuwa tofauti nitashukuru Mungu na kutafuta changamoto sehemu nyingine,”alisema Tinocco aliyechipukia kisoka katika timu ya Kagera Sugar.

Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuber Katwila alisema Tinocco amefanya vizuri msimu uliopita na yuko tayari kuendelea kufanya nae kazi msimu ujao.

“Bado lakini Tinocco ni kipa mzuri na kijana ambaye ana muda mrefu wa kucheza. Tutaona makubaliano yetu na Yanga yatakuwaje lakini tungependa kuendelea naye msimu ujao,”alisema Katwila, aliyechukua jukumu la kuinoa Mtibwa baada ya Salum Mayanga kuteuliwa kuwa kocha wa Taifa Stars.



Comments

Popular posts from this blog