HABARI, TETESI ZA USAJILI TANZANIA BARA NA ULAYA MAY 31/2017

Aguero ni moja ya wachezaji bora duniani ,  Tunamhitaji katika kikosi chetu ili kupata mafanikio ( mataji ) .  Aguero Atakuwa nasi katika msimu ujao kwani ni moja ya mchezaji muhimu kwetu " 

Hayo ni maneno ya mwenyekiti wa klabu ya manchester City ,  Emirati Al Mubarack  Akithibitisha kwamba sergio Aguero ataendelea kukipiga ndani ya manchester City msimu Ujao . 

Kauli hii imekuja muda mfupi baada ya mshambuliaji huyo kuhusishwa kutaka kuihama klabu hiyo huku tetesi zilikuwa zikidai kwamba huenda akatimkia real madrid au manchester United .

ESPN  Imemtangaza Christiano ronaldo kuwa ndiye mwanamichezo maarufu zaidi duniani kuliko mwanamichezo yeyote .  Katika listi hiyo Mcheza basketball ,  Lebron James anashika nafasi ya  2 huku Lionel messi akiwa nafasi ya 3 .

" Ni kweli nimemwambia kwamba ,  Hii ni nafasi muhimu kwake Kucheza katika timu kubwa Kwani endapo atahitaji Kujifananisha yeye na walio bora ni lazima aende kucheza katika timu bora zaidi duniani " 

Hayo ni maneno ya Arturo Vidal mara baada ya Kuhusishwa  na kutoa kauli ya  kumshawishi Alex Sanchez Aihame Arsenal na kwenda kukipiga Bayern munich .

" Zimekuja ofa  nyingi sana za vilabu mbali mbali  vikimhitaji kumsajili lakini mwenyewe amesema anahitaji kubaki ndani ya  manchester United " 

Maneno ya Wakala wa Zlatan Ibrahimovic ,  Mino Raiola .

Daniele De Rossi ameongeza mkataba wa miaka 2 ya Kuendelea kuitumikia klabu yake ya As Roma .

Maicon ametua rasmi ndani ya klabu ya Avai FC ya nyumbani kwake Brazil.

Uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspurs Umesema kwamba Upo tayari Kutoa dau la € 30m Kwaajili ya Kujaribu kunasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Attletico De madrid ,  Kelvin Gameiro . 

Uongozi huo pia umesema kwamba ,  Uamuzi wa kutaka Kumnunua mshambuliaji hiyo ni kuongoza wigo wa kikosi chao ili waweze kufanya Vizuri katika mashindano mbali mbali msimu Ujao .

Uongozi wa klabu ya Borussia dortmund umekanusha taarifa zilizoenea katika Vyombo mbali mbali vya Habari kwamba klabu hiyo imeingia makubaliano na PSG Ili kuwauzia mshambuliaji wake ,  Emerick Aubameyang . 

Dortmund wamekili kuwa mchezaji wao anatakiwa na matajiri hao wa Ufaransa ila hakuna makubaliano yeyote yaliyoingiwa baina ya timu hizo mbili mpaka sasa . 

Mapema Leo ,  vyombo mbali mbali Viliripoti Kwamba PSG na Borussia dortmund wameingia makubaliano ya kutaka kumsajili Aubameyang kwa ada ya € 61m na kukubali  kupewa kandarasi ya miaka 5 lakini Dortmund wamekanusha taarifa hizo.

Shamrashamra za michuano ya spot pesa zanukia.
Vilabu vyaendelea kujinoa.
Simba, Yanga kuwakosa nyota wake stars walioitwa Stars.

Wapingaji huwa hawakosekani
ni Mkataba wa Sportpesa wadaiwa kuanza kuzua gumzo klabuni Yanga. Baadhi ya wanachama wakitishia kwenda mahakamani.

Sportslady Shose Wazza Scholes Fidels kuagwa kesho.

Zipo taarifa zinazodai Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Azam FC, Saad Kawemba ndo basi tena hatoendelea na klab hiyo. Habar zaid zimedai hajatimuliwa kama inavyodaiwa bali mkataba wake umeisha.

Anayetajwa kama mmoja wa makocha wazawa wenye heshima zaidi nchini Mshindo Msola asema Simba inapaswa kusajili zaidi ili ishindane Kimataifa. Adokezea nafasi za golikipa, beki wa kulia, beki wa kati, viungo wawili na mshambuliaji zaid ya Mavugo

imedokezwa kumbe kabla ya kutua Singida United, kiungo Kenny Ali alizitosa Azam, Simba na Yanga.

Inadaiwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba kasema Simba kama Simba wanasubiri ripoti ya Omog ndo waanze Usajili.

mlinda lango wa Klab ya Azam FC, Aishi Manula asema Bocco alikuwa kiongozi shupavu hata hivyo amtakia heri akisema ndo maisha ya Soka.

Aliyekuwa msemaji wa Simba, Haji Manara ang'aka kwa wanaokibeza kikosi chá Simba chá Msimu uloisha.

Azam kumpa mwaka mmoja zaid kocha wake Cioaba.

Azam yaendelea na mazungumzo kuwabakiza Manula na Kapombe.

Ngoma, Niyonzima wahusishwa na Simba.

Mbaraka Yusuph aendelea kuhusishwa na Yanga.

imedaiwa mlinda lango Bathez ana uwezekano mkubwa wa kutemwa klabuni Yanga


Habari zinazodai kukamilika (Done Deals)
Arsenal imemnasa Henry Onyekuru toka Ubelgiji.

kinda toka klab ya Chelsea aitwaye Solanke kanaswa na Liverpool.

mlinda lango toka Benfica, Ederson ashawasili jijini Manchester kujiunga na klab ya Man City.

beki Matteo Mussachio kahama villareal na kutua AC Milan kwa mkataba wa miaka miwili.

AC Milan yamuongezea mkataba kocha wake, Vicenzo Montela mpk 2019.

aliyekuwa kocha msaidiz wa Luís Enrique klabun Barcelona, Unzue katua Celta Vigo

5 Tetesi za Usajili
Mousa Sissoko mbioni kutimka Tottenham.

Liverpool, PSG zadaiwa kumuwania aliyekuwa mlinzi wa Man City, Gael Clichy.

Antonio Conte adaiwa kumgeukia mlinda lango wa PSG aitwaye Alphonse Areola ili akazibe Pengo la Begovic.

Pauni milion 52 kuitoka man Utd kwa mlinz Victor Lindelof.

bosi wa Arsenal Wenger ahusishwa na Sandro Ramirez wa Málaga.

imedaiwa Jose Mourinho kashateta na Alvaro Morata.

mlinda lango Iker Casilas anaendelea kuhusishwa na klabu ya Psg.

Chelsea, Liverpool zinadaiwa kuipa upinzani klab ya Man City kunako saini ya beki wa Monaco, Benjamin mendy.

AC Milan yamtengea Alvaro Morata dau la pauni milion 60 kama ada ya usajili.


Cristiano Ronaldo asema nafsi yake inamwambia Real Madrid itashinda mfululizo Taji la Uefa. Fainali jumamosi hii.

Aliyewah kuwa mshambulizi hodari wa Arsenal, Ian Wright kasema bora Wenger alivyobakia. Mnanuna nini sasa?

KUPATA HABARI ZOTE ZA MICHEZO NA USAJILI KILA SIKU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK BOFYA HAPA

 photo nijuze habari_zpsfbogl9sm.png

Comments

Popular posts from this blog