LIPULI FC NAYO YAJA KIVINGINE, YATENGA MAMILIONI KWA AJILI YA USAJILI
Lipuli FC ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja timu nyingine mbili ni Singida United na Njombe Mji
Klabu ya Lipuli ya Iringa ambayo itashiriki Ligi ya Vodacom msimu ujao imetenga Sh. Milioni 800, kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
Mwenyekiti wa timu hiyo Abduli Majeki, amesema, mbali na kiasi hicho cha fedha pia wapo kwenye mazungumzo na makampuni matatu ili kuwadhamini katika mambo mbalimbali ya kuiimarisha timu yao kwasababu wanataka kufanya vizuri na siyo kushiriki.
“Tupo kwenye mazungumzo na makampuni matatu kwa ajili ya kutusaidia kwenye udhamini unajua tuna mkakati wa kununua basi la klabu lakini pia kufanya usajili wawachezaji wenye viwango vya juu ili kuiwezesha timu yetu kufanya vizuri hivyo lazima tuwe na pesa,”amesema Majeki.
Kiongozi huyo pia amesema wapo kwenye mazungumzo na kocha Selemani Matola, ili kuweza kuwa kocha wao baada ya kupitia CV zake na kugundua kuwa anavigezo vinavyostaili kuifundisha timu hiyo kwa kufuatilia rekodi zake katika timu alizopitia.
Amesema anatambua kuwa ligi ya Vodacom imekuwa ngumu hasa msimu uliopita hivyo nawao hilo wamelipa umuhimu mkubwa ndiyo maana wanataka kukiandaa vyema kikosi chao ili wasije kupanda na mwishoni mwa msimu wakajikuta wanashuka.
“Tuna mikakati imara sana kama itafanikiwa basi Lipuli itakuwa timu ya kutisha na tunaweza kuwashangaza watu tofauti na wanavyo fikiria, na mambo haya tunatarajia yatamalizika siku za karibuni ili zoezi la maandalizi ya timu liweze kuanza,”amesema Majeki.
KUPATA HABARI ZOTE ZA MICHEZO NA USAJILI KILA SIKU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK BOFYA HAPA

Comments
Post a Comment