Posts

Showing posts from February, 2019

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu za Inasaidia Kukufanya Uwe Rijali Bila Kuaibika Kitandani

Image
PATA TIBA YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME.INASAIDIA KUKUFANYA URUDIE MARA 5 NA KUCHELEWA KWA DK 20. TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA BAADA YA UTAFITI WA MDA MREFU JUU YA MATATIZO YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UKOSAJI WA HAMU YA TENDO LA NDOA AMA KUSHINDWA KURUDIA TENDO KWA HARAKA DR.NTOBI AMEKULETEA TIBA SAHIHI YA MATATIZO HAYO KWA KUTUMIA DAWA ZA GUMBA POWER. NI DAWA ASALI YA VIDONGE INAYOTIBU TATIZO LA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.DAWA HII INAMCHANGANYIKO WA KUTOSHA WENYE KUZALISHA VICHOCHEO VINGI VYA HEMONE ZA GESTROGEN VIKIWEMO VITAMINI B6&B1.VITAMINI E.PAMOJA NA MADINI AINA YA ZINC VITAKUFANYA KUWA NA NGUVU NA MZUNGUKO MZURI WA DAMU NA KUONGEZA HAMU NA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA ZAIDI YA HATUWA NNE AU ZAIDI .NA KUCHELEWA KUFIKA KILELENI ZAIDI YA DAKIKA 20-30 NTINJE. INARUTUBISHA MAUMBILE YA UUME YAANI KUREFISHA NA KUNENEPESHA NCHI.4-7 UPANA CM4-6 STANDARD KIAFYA HAIJALISHI UMRI WAKO HATA KWA WAZEE UKIITUMIA MAUMBILE YAKO YATAB...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 28

Image
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 28 from UDAKU SPECIAL BLOG

Steve Nyerere: Dudubaya Anapaswa Kuomba Msamaha

Image
Muigizaji nguli wa filamu nchini, Steve Nyerere, amesema kama kuna msanii anamzungumzia vibaya marehemu Ruge Mutahaba kwa sasa jkama anavyofanya Rapa Dudu Baya basi anapaswa kutengwa kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu. Steve amesema Ruge amefungua milango kwa vijana wengi na kutoa fursa waweze kufanikiwa huku akiweka wazi kuwa atamkumbuka milele. from UDAKU SPECIAL BLOG

Serikali yalipiga 'STOP' gazeti la The Citizen

Image
Serikali imesimamisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa muda wa siku 7 kuanzia leo Jumatano. Serikali imedai Februari 27lilichapisha habari ya upotoshaji kuhusu maoni ya wataalamu waliozungumzia kuporomoka kwa shilingi iliyochapishwa Februari 23, 2019. from UDAKU SPECIAL BLOG

Watu 7 Wafikishwa Mahakamani Mauaji ya Watoto Njombe

Image
Watu saba wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe  kwa tuhuma za mauaji ya watoto mkoani Njombe yanayohusishwa na imani za kishirikina. Mmoja wa watuhumiwa hao ni David Kasila ambaye alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe februari 18 mwaka huu akituhumiwa kuwaua watoto watatu ambao ni Oliver Ng’ahala(5),Goodluck Mfugale(5)Meshack Myonga(4) wote ni wakazi wa wilaya ya Njombe. Watuhumiwa wengine ni Mariano Malekela,Edwini Malekela,kalistus Costa wakazi kijiji cha Matembwe tarafa ya Lupembe walifikishwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe mnamo februari 19 mwaka huu kwa tuhuma za kumuua mtoto wao Rachel Malekela(7) februari moja mwaka huu ambapo mwili wake ulikutwa mita 50 kutoka nyumbani kwao akiwa amechinjwa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Renata Mzinga,alisema kati ya watuhumiwa 49 waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi baada upelelezi watuhumiwa saba pekee ndio walik...

Waziri Makamba Aandika Waraka Mzito....."Ruge, naomba nisikilize kidogo. "

Image
Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia. Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona — hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako. Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali...

CHADEMA watuma salamu za pole kwa familia ya Ruge Mutahaba

Image
Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) limetuma salamu za Pole kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba kilichotokea siku ya jana. from UDAKU SPECIAL BLOG

Msiba Hautakuwa wa majonzi kama Bali Itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka Iwe- Kusaga

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema kwamba msiba wa Ruge hautakuwa wa majonzi kama ilivyozoeleka, bali itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka iwe. Kusaga amezungumza hayo akisema kwamba kabla Ruge hajafariki, aliwahi kusema kuwa ikitokea siku amekufa, basi watu wasihuzunike sana, bali washerehekee maisha yake na vile alivyo vifanya wakati yupo hai. “Kuna kitu alikuwa akisisitiza, kwamba ikitokea bahati mbaya Mwenyezi Mungu amemchukua, tu-'celebrate' maisha yake, tu-'celebrate' alivyovifanya,  kwa hiyo tutaanza maombolezo lakini yatakuwa ku-'celebrate' mazuri aliyoyafanya, hii alisisitiza wazi kabisa, na mimi kumpa heshima hiyo ni lazima tu-'celebrate' mengi mazuri aliyoyafanya”, amesema Kusaga. Akiendelea kuzungumzia hilo Joseph Kusaga amesema kwamba Ruge amefanya mengi mazuri ambayo yalifaa kutunukiwa, huku akitoa shukrani kwa serikali kwa kuwa nao bega kwa bega, kwenye kipindi hiki kigumu ...

Walioigiza sauti ya Rais kutapeli wakamatwa

Image
Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali. Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni Mwenyekiti wa Sameer Africa, aliigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara. Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi  huku vyombo vya habari nchini Kenya vikitofautiana kwamba ni shilingi milioni 10, huku gazeti lingine likiandika kwamba ni shilingi milioni 80. “kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano ya simu”, ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation. Wakati wa operesheni hiyo, polisi walikamat...

Dudu Baya amjibu Waziri Mwakyembe kuhusu kukamatwa ‘nakuja mwenyewe nielekezeni kituo Gani nifike Msichome Mafuta"

Image
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya amemjibu Waziri Mwakyembe aliyetaka Jeshi la Polisi limkamate kwa kosa la kumdhihaki marehemu Ruge Mutahaba. Dudu Baya kupitia video aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, amemtaka Waziri Mwakyembe kutosumbua Askari, bali wamwambie ni kituo gani anatakiwa akaripoti na yeye yupo tayari. Mapema asubuhi ya leo Februari 26, 2019. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameliomba BASATA kumchukulia hatua Dudu Baya na Jeshi la Polisi limkamate. from UDAKU SPECIAL BLOG

Hii Hapa Ratiba ya Mazishi ya Ruge Kuzikwa Kwao Bukoba Jumatatu

Image
NDUGU Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa #RugeMutahaba utawasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya IJUMAA (March 1/2019). Ikiwa hivyo wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga mpendwa wetu siku ya JUMAMOSI (March 2/2019). . Baada ya hapo: Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya JUMATATU (March 4/2019) (Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba) from UDAKU SPECIAL BLOG

Uwanja wa ndege wa kisasa kujengwa Pemba

Image
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatarajia kujenga Uwanja wa ndege wa kisasa kisiwani Pemba utakaoruhusu kutua ndege kubwa. Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, aliyasema hayo Wawi Chake Chake Pemba, wakati wa majumuisho ya ziara yake kisiwani humo. Alisema kuwa Uwanja huo utakuwa wa kisasa na mkubwa utakaoruhusu ndege za aina zote kubwa kutua katika kiwanja hicho na kusaidia usafiri wa anga. Alisema tayari mchakato wake umeanza na ameshatuma mawaziri 10 kwenda kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya pembezoni mwa Uwanja huo wakiwamo wananchi wa Mfikiwa, Furaha na Mvumoni ili wakae tayari ujenzi utakapoanza waweze kuondoka katika eneo hilo na kupewa fedha kwa ajili ya mali zao. Dk. Shein alisema kuwa tayari upembuzi yakinifu umeshafanywa kwa ajili ya uwanja huo mpya wa ndege na karibu Sh. milioni 500 zimetumika na hivi sasa serikali iko katika hatua za kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi huo. “Niwaombe wananchi kuwa na subira hasa wale wanaoishi pembezoni mwa uwa...

Waziri Mkuu Atua Msibani Kutoa Pole...... Amzungumzia Ruge

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefika kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG) ambaye amefariki siku ya jana. Kwa niaba ya serikali Waziri Mkuu amesema kuwa Ruge alikuwa mwenye mchango mkubwa sana ndani ya serikali na taifa kwa ujumla. "Marehemu ndani ya Serikali amefanya kazi kubwa sana kwa kutafsiri philisophia ya viongozi wetu. Alianza awamu ya Nne (chini Rais Mstaafu Dkt Kikwete) na awamu hii ya tano...Amefanya kazi kubwa ya kuelimisha, ametoa mchango mkubwa wakati mwingine hata wa fedha zake." Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Ameendelea kwa kusema, 'Kwa niaba ya Serikali, kwa niaba ya Rais Dkt Magufuli ambaye anaendelea na itifaki zake lakini atakuja, nimekuja kutoa salamu za awali,'. Ruge Mutahaba amefariki siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini. from UDAK...

Serikali Yashikilia Msimamo wake Kuhusu Mgodi wa North Mara

Image
Serikali kupitia Wizara ya Madini imesema bado imeshikilia msimamo wake kuhusu muda uliotolewa kwa Mgodi wa North Mara kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa kwenye kikao cha Januari 9, 2019 kuhusu Bwawa la kuhifadhi topesumu (Tailings Storage Facility -TSF). Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila Februari 26, 2019 wakati akizungumza katika mahojiano maalum ofisini kwake Jijini Dodoma, mara baada ya kufungua kikao cha pamoja baina ya wajumbe kutoka serikalini na wajumbe kutoka Mgodi wa North Mara waliokutana kujadili kuhusu hatua zilizofikwa na Mgodi katika kutekeleza maagizo hayo. Amesema serikali haitoongeza muda zaidi ya ule uliotolewa katika kikao cha awali, na kusema kuwa msimamo wa serikali utabaki kuwa hivyo.  “Ndugu zangu katika kikao hiki kilenge kutoa majibu ya utekelezaji wa maagizo ya serikali kama yalivyowasilishwa kwenye kikao cha Januari 9, 2019, ni kwa kiasi gani mmetekeleza maagizo hayo,” alisema Prof. Msanjila. Seri...

VIDEO: Kwaniaba ya CCM tunapenda kutoa pole kwa familia ya Ruge - Humphrey Polepole

Image
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akizungumzia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye amefariki hapo juzi, February 26 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI, PIA SUBSCRIBE.......... from MUUNGWANA BLOG

VIDEO: Alichozungumza Ommy Dimpoz Msibani kwa Ruge Mutahaba

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akizungumzia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye amefariki hapo juzi, February 26 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI, PIA SUBSCRIBE.......... from MUUNGWANA BLOG

VIDEO: Masoud Kipanya atoa siri nzito kuhusu Ruge Mutahaba

Image
Mtangazaji wa Clouds FM, Masoud Kipanya akizungumzia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye amefariki hapo juzi, February 26 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI, PIA SUBSCRIBE...... from MUUNGWANA BLOG

RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

Image
MKUU WA CHUO CHA RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA ANATANGAZA KUPOKEA MAOMBI KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020 KWA INTAKE YA MARCH-APRIL  KATIKA KOZI ZIFUATAZO:  1. ORDINARY DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (AFISA TABIBU) MIAKA 3 SIFA ZA MWOMBAJI:  AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO FIZIKIA'D' BIOLOJIA'D' KEMIA’D’ NA IKIWEMO HESABU NA ENGLISH NI KWA NYONGEZA KWA MASOMO MOJAWAPO.  2. CETIVICATE IN IN CLINICAL MEDICIN (AFISATABUBU MSAIDIZI) MIAKA MIWILI SIFA ZA MWOMBAJI:  AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA MASOMO ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO MASOMO YA FIZIKIA'D' BIOLOJIA 'D' CHEMIA'D' NA IKIWEMO HESABU NA KINGEREZA KWA MASOMO MOJAWAPO 3. CETIVICATE IN IN COMMUNITY HEALTH (UHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII MWAKA MMOJA  SIFA: AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA MASOMO ANGALAU AWE AMEPATA 'D' NNE IKIWEMO SOMO LA BIOLOJIA YOTE HAYA YANAZINGATIWA MWONGOZO WA WIZARA YA AFYA NACTE CHUO KIMESAJILIWA KWA...