Usajili Yanga: Wanaoingia, wanaobakizwa na wanaotemwa 2017/18
Wakati dirisha la usajili na uhamisho wa wachezaji Ligi Kuu Tanzania Bara, tayari Mabingwa watetezi, Yanga wameanza kufanya biashara ya kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu jao. Mazungumzo kati ya Yanga na beki wake kisiki, Vincent Bossou yanaonekana kukwama na tayari viongozi wa klabu hio wameinua mikono. Bossou alijiunga Yanga mwaka 2015 akitokea ligi daraja la pili Korea Kusini. Mshambuliaji Malimi Francis Busungu ameoneshwa mlango wa kutokea baada ya kumaliza msimu kwa kucheza mechi moja tu ya ligi ambayo hata hivyo alipumzishwa baada ya dakika 32 tu za kipindi cha kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar. Kiungo mkabaji, Justine Zulu anaripotiwa kuwa mbioni kutemwa na Yanga. Zulu alisajiliwa wakati wa dirisha dogo lakini baada ya kucheza mechi 8 tu za Ligi anaonekana kutokuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha kwanza. Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe naye ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akifuata nyayo za Donald Ngoma. Msha...