Emmanuel Okwi: nyie chongeni, lakini mjipange kwelikweli

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Emmanuel Okwi ameweka wazi mipango yake ya msimu ujao kwamba amekuja Simba kufanya kazi kwani ndicho kinachomleta katika kikosi cha timu hiyo kitakachokuwa na ushindani mkali msimu ujao.

Okwi raia wa Uganda aliwasili nchini mapema wiki hii na kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Villa SC ambayo alikuwa akiichezea kwa lengo la kurudisha kiwango chake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiwa Denmark ambako alivunja mkataba na timu ya Sønderjyske.

Okwi amesema kuwa matarajio yake ni kucheza soka safi na amekuwa akiifuatilia  Simba kwa kipindi kirefu ambapo amegundua kuwa kuna nyota wazuri ambao wakishirikiana kwa pamoja watafanya mambo makubwa kwa timu hiyo.
“Nimejipanga, naamini kiwango changu kimerejea kwani awali nilijiona kabisa kuwa nimeshuka na ndiyo maana nilisaini mkataba mfupi na Villa, timu ambayo imenilea vizuri. Kuja kwangu Simba si kwamba ni miujiza bali ni makubaliano yaliyokuwepo toka mwanzo yaani tangu nilipovunja mkataba Denmark.
“Kwa sasa mimi ni Okwi mwingine ingawa najua wengi watakuwa na matarajio tofauti na mimi, Okwi huyu sio yule wa zamani, najitambua na ninajua nini nafanya katika kazi yangu, nimesaini Simba na ninaipenda, Simba ni kama nyumbani kwani wamekuwa wakinilea vizuri,” alisema Okwi.

Kwa mujibu wa Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa baada ya kusaini mkataba huo,  Okwi atajiunga na kikosi chao mapema mwezi ujao ambapo kitaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na baadaye watahamishia kambi yao nje ya Dar es Salaam. Simba hupendelea kuweka kambi yao mjini Morogoro.

Kupata habari zetu bure kila siku Download Application yetu Bure GUSA HAPA pia usikose kutufatilia kila siku SISI NI SOKA TUNAENDELEA KUKUJUZA.

Comments

Popular posts from this blog