Tetesi za Usajili Barani Ulaya leo Ijumaa ya tarehe 30 June 2017

Mtoto wa Zinedine Zidane, Enzo ameondoka Real Madrid kwenda kujiunga na Alaves. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 22, amesaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kushindwa kupata nafasi ya uhakika katika timu inayosimamiwa na baba yake. (Chanzo FourFourTwo)
Liverpool wako tayari kupanda dau kwa kiungo wa RB Leipzig anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 70 Naby Keita, 22. (Chanzo Mirror)
 Majogoo hao wa Jiji wanamatumaini ya kuwapata kwa pamoja kiungo huyo wa kimataifa wa Guniea na kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Chanzo Liverpool Echo)
Everton watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Malaga Sandro, 21, wiki ijayo. Everton walifikia dau la mchezaji huyo na tayari alisha pass vipimo vya matibabu lakini klabu ya Hispania haitaki kumruhusu hadi mkataba wake utakapoisha tarehe 3 Julai. (Chanzo Liverpool Echo)
Manchester United haitamuuza Ander Herrera kwa Barcelona msimu huu wa majira ya joto, licha ya ripoti kudai klabu hiyo ya Hispania itazingatia kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa itashindwa kumpata kiungo mwenzake Marco Verratti, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Paris St-Germain. (Chanzo Independent)
Chelsea inataka kumsajili beki wa Roma Kostas Manolas. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alikaribia kuhamia Zenit St Petersburg kwa paundi milioni 26 lakini amesimama ili kuangali nafasi nyingine. (Chanzo London Evening Standard)
 Southampton wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho, 20, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25. (Chanzo Sun)
Kocha wa Watford Marco Silva anataka kumsajili Kieran Gibbs kutoka Arsenal. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amehusishwa pia na Liverpool. (Chanzo Mirror)
Monaco haitarajii kumuuza Thomas Lemar msimu huu wa majira ya joto na wamekwisha waambia  Arsenal na Tottenham, kuwa winga huyo mwenye umri wa miaka 21, hayuko sokoni. (Chanzo Independent)
Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis anasema klabu hiyo itafanya usajili zaidi msimu huu. (Chanzo Star)
Mwenyekiti wa West Ham, Daudi Dhahabu amekanusha taarifa za klabu hiyo kumfukuzia mchezaji wa Arsenal Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 25, na anasema klabu hiyo inatafuta washambuliaji wawili wapya wenye uzoefu na Premier League. (Chanzo Talksport)
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amepost picha ya akiwa amebeba watoto wake mapacha. “Nina furaha sana kuweza kubeba wapenzi hawa wapya wawili wa maisha yangu,” aliandika mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.
Wachezaji wa Barcelona wa zamani na wa sasa wameanza kuwasili nchini Argentina kwa ajili ya harusi ya Lionel Messi. Mshambuliaji huyo wa Barca amewaalika wachezaji kama Cesc Fabregas, Samuel Eto'o na Carles Puyol. (Chanzo Mail)

Comments

Popular posts from this blog