Katiba ya Simba inasemaje kuhusu hatma ya Aveva, Ismail Adden Rage kaeleza yote hapa
Juni 29, 2017 viongozi wa juu wa klabu ya Simba Rais wa klabu Evans Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya TAKUKURU kuwashikilia viongozi hao kwa siku kadhaa, viongozi hao wamesomewa mashtaka matano yakiwemo ya kughushi nyaraka ili kujilipa deni ambapo inadaiwa waliikopesha Simba dola za Marekani 300,000 huku makosa mengine yakiwa ni ya utakatishaji pesa.Swali linakuja kwamba, inapotokea viongozi wa ngazi ya juu kama hao wa Simba kushikiliwa na mahakama jukumu la kuiongoza klabu linakuwa kwa nani?
Ismail Adden Rage ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo kwa mujibu wa katiba ya Simba anayoifahamu yeye kama haijabadilishwa.
“Katika ali kama hii viongozi wa kamati ya utendaji watakaa wajitathmini ni nani miongoni mwao ambaye ni senior anaweza akakaimu kwa uda lakini badae itabidi waitishe mkutano mkuu ili waweze kuamua lakini katiba haisemi itachukua muda gani kufanya hivyo lakini pia katiba hairuhusu sana kukaimu bila kupata baraka za mkutano mkuu.”
“Ni vyema kamati ya utendaji ikakaa na kusoma katiba vizuri, kama haijabadilishwa ninavyofahamu mimi, endapo Rais hayupo basi madaraka yote yatachukuliwa na makamu wa Rais endapo pia kakamu wa Rais hayupo, miongoni mwa wale wajumbe wa kamati ya utendaji ambaye ni senior kuliko wote ataongoza klabu hadi hapo mkutano mkuu utakapoamua vinginevyo kama haijabadilishwa.”
Kama ikitokea viongozi hao wakatiwa hatiani kwa makosa yanayo wakabili halafu wakatoka Rage ameendelea kufafanua kama viongozi hao watakuwa na sifa ya kuendelea kuongoza au ndio utakuwa mwisho wao.
“Huruhusiwi tena kuwa kiongozi katika klabu yoyote ile, vilabu vya mpira vyote vimesajiliwa kwa msajili wa vyama vya michezo, mimi binafsi nimewahi kupata matatizo lakini kwa bahati nzuri mahakama ya rufaa ilinisafisha. Kwa kuwa mahakama ya rufaa ilinisafisha, basi kwa maana hiyo katika maisha yangu bado sijawahi kutiwa doa mahali popote.”
Comments
Post a Comment