Dondoo za Usajili Tanzania na nje ya Tanzania
Hatma ya Haruna Niyonzima Kujulikana wiki Ijayo , Simba yasema Haiwezi Ongelea Juu ya hilo tena kwani mwenye macho ataona na mwenye masikio atasikia .
Ndanda FC imesema kwamba Wataangalia Uwezekano Wa Kumnasa , Julio awe kocha wao mkuu .
Yanga yasema bado Hawajamaliza Usajili , Wasikika wakisema Watashusha Vifaa pale Itakapo bidi .
Mkude asema Kwamba Hawezi kuongelea sana Usajili Unaofanywa Klabuni hapo ila muda Utaongea .
Za kimataifa
Sunderland imemtangaza Simon Gryson kuwa kocha mkuu Wa Klabu hiyo na kumpa kandarasi ya miaka 3 .
Klabu ya Deportivo Alaves ya nchini Hispania imefanikiwa kunasa Saini ya mtoto Wa kocha Zinedine Zidane Wa kuitwa Enzo Zidane na kumpa kandarasi ya miaka 3 akitokea Real Madrid .
Chelsea Kukamilisha Usajili Wa Kiungo Wa Monaco ya Ufaransa , Bakayoko siku ya Kesho huku Ikisemekana Huenda wakapiga " Double tap in one top of bottom " Kwa kumsainisha Alex Sandro .
Malaga Imenasa Saini ya miaka 3 ya Adrian Gonzalez akitokea Eibar .
Klabu ya arsenal inaanda ofa Kwaajili ya kunasa Saini ya beki Wa Klabu ya OGC Nice , Jarden Dalbert .
Wesley Sneijder huenda Akatimkia ndani ya Klabu ya sampdoria ya nchini Italia Mara baada ya Kuingia makubaliano na Wakata Ufuta hao Wa Jiji la Italia .
Suso Wa Ac Milan amesema kwamba mpaka sasa amepokea ofa kubwa 3 toka katika Vilabu vinavyoshiriki Ligi ya mabingwa BARANI Ulaya , lakini ameamua Kubaki kuichezea Ac Milan msimu Ujao .
FC Barcelona imefikia makubaliano na Klabu ya Real betis Ili kuwauzia kinda wake , Christian Tello Huku € 7M zikiwa ada ya Uhamisho wake na atakula kandarasi ya miaka 4 .
Baada ya Juventus Kuthibitisha kwamba Dani alves anaihama Klabu hiyo , Manchester City imesema ipo tayari kutoa dau lolote ili kunasa Saini ya mkali huyo.
Westbrom inasubiri majibu toka Klabu ya Intermilan mara baada ya kupeleka dau la € 5M ili kunasa Saini ya beki , Andrea Ronacchia .
Baada ya Dani alves Kutimka ndani ya Juventus , Klabu hiyo imeandaa ofa ya € 15M + Bonus ili kunasa Saini ya Danilo Wa Real Madrid kama mziba pengo hilo .
Manchester City wapo katika meza ya mazungumzo na klabu ya Tottenham ili kuangalia Uwezekana Wa kunasa Saini ya beki wake , Kyle Walker .
Klabu za FC Barcelona na Manchester City wote wapo katika mbio za kutaka kunasa Saini ya Ousmane Dembele Wa Borussia Dortmund , Dortmund wamesema thamani ya mchezaji huyo ni € 85M .
Klabu ya Liverpool imesema kwamba bado watahitaji Saini ya Aubameyang ili kujiimalisha zaidi , Kuhusiana na Upande Wa beki Klabu hiyo imesema IPO katila rada za hali ya Juu ili kuangalia Kifaa Kitakacho stahiki Kujenga Ukuta Wa Klabu hiyo .
Belhanda na Bafetimbi Gomis ni Mali ya Galatasaray kwa sasa .
Jermain Defoe ni Mali ya Bournemouth .
Fabio Borini ni Mali ya Ac Milan kwa sasa .
Kupata habari zetu Bure kila siku Download Application yetu Bure GUSA HAPA pia usikose kutufatilia kila siku SISI NI SOKA TUNAENDELEA KUKUJUZA.
Comments
Post a Comment