Hiki ndicho alichokisema Mayanja baada ya Simba kutua Z’bar
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amewaambia wanachama na mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yao kwa ajili ya kuendeleza moto waliotoka nao ligi kuu Tanzania bara kwenye michuano ya Mapinduzi. “Wanasimba waje kwa wingi kuishangilia timu yao kuendeleza mwendo wetu tuliokuwa nao kwenye Vodacom Premier League.” “Kikosi cha Simba chote ni cha kwanza hakuna tunachezesha kila mchezaji hakuna kikosi cha kwanza, ni muda tu wa kubadilisha kidogo-kidogo.” Simba ndio timu ya kwanza kufika visiwani Zanzibar kutoka Tanzania bara ambapo iliwasili asubuhi kwenye Bandari ya Zanzibar.