Simba Sports Club :TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Simba Sports Club
D'salaam, Tanzania
30th Dec 2016.
Klabu ya Simba imepokea kwa mstuko mkubwa taarifa ya msiba wa watoto wa mchezaji wetu Juuuko Murshid vilivyotokea leo huko kwao nchini Uganda.
Vifo vya watoto hao watatu vimekuja katika kipindi hiki ambapo mchezaji wetu huyo wa kimataifa, akiwa kwenye maandalizi ya fainali za mashindano ya Afcon, yanayotarajia  kuanza katikati ya mwezi ujao.

Tunajua uzito wa kufiwa na na watoto hao, na tunatambua uchungu aliona nao nyota wetu huyo, yeye pamoja na mkewe, lakini tunaamini Mungu atawapa subira na uvumilivu mkubwa ktk kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Mwisho klabu inawatakia Wanasimba na Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2017.
Imetolewa na. *Haji S Manara*
Mkuu wa Habari wa Simba Sc

Comments

Popular posts from this blog