Aliyemchoma mkulima mkuki mdomoni akamatwa


 Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi kwenye mamlaka husika na hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa.

Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na kuomba hifadhi kwa wasamaria wema.

Source: ITV

Comments

Popular posts from this blog