Pierre Emerick-Aubameyang, 28, anayenyatiwa na Liverpool anaonekana kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Tianjin Quanjian ya China, ambayo imetoa dau la pauni milioni 70 (Daily Star). Manchester City sasa wanaongoza katika mbio za kumsajili Alexis Sanchez, 28, baada ya Bayern Munich kujitoa kutokana na bei kubwa ya mchezaji huyo wa Arsenal (Daily Mirror). Manchester City wana uhakika wa kumsajili Alexis Sanchez kwa takriban pauni milioni 50, kwa sababu ya hamu ya mchezaji huyo kufunzwa na Pep Guardiola (Guardian) Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-Germain katika kumsajili beki Alex Sandro, 26, huku Juventus wakitaka pauni milioni 61 (Daily Mail). Chelsea wanatazamiwa kukamilisha usajili rasmi wa Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco wiki hii (The Sun). Wakala wa kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Spain (Marca). Manchester United watazidiwa kete na Paris St-Germain katika kumsajili ...