Taifa Stars yaifuata Afrika Kusini, ni baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Mauritius.
Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuingia hatua ya Robo fainali ya kombe la Halmashauri ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa miguu kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya Kulazimisha kwenda Sare ya 1-1 dhidi ya Mauritius kwa goli lililofungwa na Simon msuva dakika ya 68' dakika moja tu baada ya Mauritius kuandika goli la kuongoza (dk 67') kupitia kwa Kelvin Perticots, huku Angola nayo ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Malawi.
Kwa matokeo hayo Tanzania inaongoza kundi 'A' kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Angola ambayo nayo ina alama sawa na Tanzania
FT: Tanzania 1 - 1 Mauritius
FT: Malawi 0 - 0 Angola
Tanzania itakutana na Afrika Kusini katika Mchezo wa Robo Fainali tarehe 5 July.
Nijuzehabari inaungana na watanzania wote kuitakia kila la kheri timu yetu ya Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Taifa Stars.
Kupata habari zetu kila siku Download Application yetu Bure GUSA HAPA pia usikose kutufatilia kila siku SISI NI SOKA TUNAENDELEA KUKUJUZA.


Comments
Post a Comment