Taifa Stars Kuzisaka Pointi 3 leo Dhidi ya Mauritius

Timu ya taifa ya Tanzania leo tena inajitupa uwanjani kusaka nafasi ya robo fainali dhidi ya Mauritius.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 12 kamili jioni kwa saa za hapa nyumbani. 

Stars imekuwa na maendeleo mazuri katika michuano hiyo ikianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Malawi na kutoka sare tasa na Angola. 

Stars wanaongoza kundi A kwa tofauti ya magoli wakiwa na alama 4 sawa na Angola . Mauritius nafasi ya tatu na Malawi wakiwa mkiani lakini wote wakiwa na alama 1. 

Kila kundi linatoa timu moja kuingia hatua ya robo fainali hivyo kama Stars itafanikiwa kushinda leo kwa idadi kubwa ya magoli itajiweka katika nafasi nzuri ya kuingia robo fainali. Kupoteza kwa Angola au kushinda kwa idadi ndogo ya magoli kwa Angola dhidi ya Malawi ni furaha kwa Tanzania endapo watashinda mchezo wao.

Ushauri wangu kwa Kocha wa Taifa stars Salum Mayanga amwanzishe Mbaraka Yusuph na kumpumzisha Elias Maguli katika ushambuliaji kwa sababu Mbaraka mpira anaoucheza unaonesha ni bora zaidi ya Maguli endapo tunataka kushinda basi kikosi kikae vile vile mabadiliko yafanyike kwa mtu mmoja tu ni ushauri tu.

Hivi karibuni tutakuwekea Kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza dhidi ya Mauritius

Kupata habari zetu kila siku Download Application yetu Bure GUSA HAPA pia usikose kutufatilia kila siku SISI NI SOKA TUNAENDELEA KUKUJUZA.


Comments

Popular posts from this blog

Njia sahihi za kuachana na unywaji wa pombe