Posts

Showing posts from June, 2019

Taliss-IST yachangia timu za Taifa za mchezo wa kuogelea

Image
Waogeleaji wa timu ya Taliss-IST wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki katika mashindano maalum ya kuzichangia fedha timu za Taifa za mchezo wa kuogelea ili zishiriki katika mashindano ya Dunia.    Dar es Salaam. Mabingwa wa mchezo wa kuogelea nchini, Taliss- IST ya Upanga imechangia kiasi cha Sh1.5 millioni kwa ajili ya timu za taifa za mchezo huo zinazojiandaa na mashindano ya Dunia mjini Gwangju, Korea Kusini na mashindano ya vijana ya dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Budapest, Hungary.  Klabu hiyo iliwakilisha fedha hizo katika mashindano maalum yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert yaliyoandaliwa na Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA).  Taliss-IST ilichangia fedha taslimu Sh1,225,000 na dola za Kimarekani 140 katika mashindano hayo maalum ambayo yalishirikisha waogeleaji wenye umri tofauti.  Waogeleaji hao hao ni Mohameduwais Abullatif, Lara Steenkamp Aravind Raghavendran, Fallih Ahmed, Ahme...

DAR ES SALAAM NA TABORA ZATWAA UBINGWA WA MPIRA WA KENGELE

Image
Washiriki wa mchezo wa mpira wa Kengele na mabingwa wapya timu ya mpira wa kengele kutoka mkoa wa Tabora wasichana wakiwa katika mchezo wa fainali dhidi ya Morogoro ambapo matokeo Tabora 16- 7  Baadhi ya wachezaji wa soka maalum wakipambana vikali kuingia hatua ya nusu fainali baina ya timu za mikoa ya Dodoma na Simiyu. ………………………….. Na Mathew Kwembe, Mtwara Timu ya wavulana kutoka mkoa wa Dar es salaam na timu ya wasichana kutoka mkoa wa Tabora zimefanikiwa kujishindia nafasi ya kwanza baada ya kufanikiwa kuwabwaga wapinzani wao katika kuwania ubingwa wa mpira wa kengele katika fainali za UMITASHUMTA zilizofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. Timu ya wavulana kutoka mkoa wa Dar es salaam ndiyo ilikuwa ya kwanza kufanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Lindi 23-13, huku mshindi wa tatu kwa upande wa wavulana ilikuwa timu ya Tanga baada ya kuifunga Tabora 14-7. Kwa wasichana Tabora ilishika nafasi ya kwanza baada ya kuilaza Morogor...

WAZIRI KAIRUKI AUTAKA UONGOZI WA KNAUF KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII INAYOWAZUNGUKA

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia moja ya malighali zinazotumika katika kiwanda cha KNAUF (Metal Profile) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda hicho na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo. Meneja Uzalishaji Bw. Nurdin Bofu akimuonesha jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara kuhusu namna wanavyopakia unga maalumu wa kutengeneza jasi wakati wa ujenzi wakati wa ziara yake. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalai moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda kinachotengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo. ...

WAZIRI MHAGAMA AKABIDHI VIFAA VYA KUTEMBELEA KWA WALEMAVU

Image
Na Charles James wa Michuzi TV  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapata huduma bora zinazowahusu bila changamoto yoyote. Waziri Jenista ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa vya kutembelea Baiskeli 'wheelchair' na fimbo kwa watu wenye ulemavu mkoani Dodoma. " Niwapongeze sana Kampuni ya Sigara nchini TCC kwa kuandaa tukio hili sambamba na kugawa vifaa hivi maalumu vya kutembelea kwa ndugu zetu wenye ulemavu. " Hii ni kumuunga mkono Rais wetu Dk John Magufuli katika kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu ambapo tumeshuhudia katika Serikali yake akiteua watu wenye ulemavu kushika nafasi mbalimbali," amesema Waziri Jenista. Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa amemshukuru Waziri Jenista kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la makabidhiano ya vifaa hivyo...

Lazaro Nyalandu Asema ni Aibu kwa Tanzania Lissu Kufutiwa Ubunge

Image
Dar es Salaam. Waziri wa zamani wa maliasili na utalii nchini Tanzania, Lazaro Nyalandu amesema uamuzi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wa kutangaza kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kilichokuwa kikiongozwa Tundu Lissu kiko wazi. Spika Ndugai alitangaza uamuzi huo jana bungeni akisema hafahamu mbunge huyo aliko na hajajaza fomu za madeni na mali za viongozi wa umma. Nyalandu ambaye alikuwa mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM alijiuzulu ubunge na kuhamia Chadema Oktoba 30 mwaka 2017. Katika ukurasa wake wa akaunti ya Twitter aliandika maandiko mbalimbali kuhusu Lissu kupoteza ubunge wake. “Kitendo cha Mh. Spika kumvua Ubunge Mh. @tundulisu huku akiwa anaendelea na matibabu Ubelgiji kufuatia shambulio dhidi yake la kupigwa risasi ni aibu na fedheha kwa demokrasia. Tundu Lissu ameonewa sana, haipendezi kuendelea kumuumiza zaidi. Hakika haki huinua Taifa. #BungeTZ.” Ujumbe mwingine wa Nyalandu ulisema, “Mbunge wetu #SingidaMashariki. #TunduLissu. Tunaendelea kukuo...

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI HOSPITAL YA BENJAMIN

Image
Na Charles James wa Michuzi Tv- Dodoma TAASISI  ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa imefungua na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi ikiwa ni mara ya kwanza yangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo kubwa nchini. Akizungumza na wafanyakazi wa Hospital hiyo, Katibu Mkuu Wizara  ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula ametoa rai kwa Wafanyakazi wa baraza hilo kuwajibika na kufanya kazi kwa kujituma zaidi pamoja na kuonesha uzalendo kwa Wagonjwa. “Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma atatizimiza wajibu  wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa. Hakuna kazi  ya neema na ibada tunayo fanya kama hii, Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au saa 1 jioni una dhambi gani.” Amesema Dk Chaula. Aidha amewataka wafanyakazi...

NAIBU WAZIRI KANYASU AIPONGEZA TFS, ATAKA MATUMIZI SAHIHI YA BOTI

Image
Na Ripota wetu ,wa Michuzi TV NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amezindua boti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko. Pia Kanyasu ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu nchini. Akizungumza leo Jumamosi Juni 29,2019 wakati wa uzinduzi boti hizo Kanyasu ameitaka TFS iongeze bidii kwa  kubuni matumizi  sahihi ya  boti hizo. "Kumekuwa na matumizi tofauti na yaliokusudiwa hivyo inabidi kubuni matumizi na kuwa na nidhamu katika matumizi yaliyokusudiwa" amesema Kanyasu. Amesema boti hizo zitasaidia kuthibiti  uvunaji holela wa mikoko ambayo ni muhimu kutokana na uhifadhi wa bahari. Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TFS Meneja Kanda ya Mashariki, Caroline Malundo amesema boti hizo zitatumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko na kuongeza kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya hifadhi ikiwemo ukataji wa mikoko na kufanya kilimo cha mpunga...

DIWANI YINDI AJA NA MPANGO WA KUKUZA MICHEZO DODOMA

Image
Na Charles James,Globu ya jamii Katika kukuza vipaji vya vijana katika Mkoani Dodoma, Diwani wa Kata ya Buigiri iliyopo Wilaya ya Chamwino Kenneth Yindi ameandaa mashindano ya mpira wa miguu yatakayoshirikisha tmu mane za kata hiyo. Mashindano hayo yaliyopewa jina la Buchimwe Cup 2019, yatazinduliwa kesho na Mkurugenzi wa Michezo Nchini, Ado Komba ambapo mshindi wa kwanza atajnyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu. " Lengo la mashindano haya ni kukuza vipaji vya vijana wetu, Michezo imekua Ajira kubwa Duniani kote hivi sasa, hivyo kama Diwani nimeoana nianzishe mashindano haya ambayo naamini yatatumika kama fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata Timu kubwa zaidi ya hizi walizonazo sasa. "Tunashukuru Wizara ya Michezo chini ya Waziri Mhe Harrison Mwakyembe kwa kutuunga mkono katika kufanikisha mashindano haya bila kuwasahau Chama Cha Soka Mkoa (DOREFA)," amesema Yindi. Ameongeza licha ya Ligi hiyo kuchezwa pia ameandaa mafunzo ya uamu...

Kocha Mwinyi Zahera agoma kurejea Tanzania

Image
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma kurudi mapema Bongo endapo timu ya taifa ya Congo itapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zimbabwe katika michuano ya AFCON 2019 inayoendelea nchini Misri. Zahera kwa sasa yupo na kwenye benchi la ufundi la timu ya Congo akiwa ni kocha msaidizi na timu yake ipo mkiani kwenye kundi A baada ya kupoteza michezo yote miwili kwa kufungwa na Uganda pamoja na Misri. Zahera amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurejea Tanzania kuanza kukikonoa kikosi chake cha Yanga badala yake atakwenda Ufarasa kula bata na familia. “Nimkekaa muda mrefu Tanzania nikiwa na timu yangu ya Yanga, kwa sasa sifikirii kurejea mapema kuanza maandalizi kwani ni muda wangu wa kupumzika na mke wangu. “Mchezo wangu wa mwisho utakuwa tarehe 30 nina imani ya kufanya vizuri kwani tayari kwa sasa wachezaji wamepata uzoefu na nina imani ya kushinda kama tukipoteza basi nitakwenda zangu Ufarasa kupumzika na familia,” amesema Zahera. from UDAKU SPECIAL BLOG

WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MTAA MNAALIKWA KUSHIRIKI NA KUSHUHUDIA UWEKAJI SAINI MIRADI MIKUBWA YA USAMBAZAJI MAJI

Image

SERIKALI YADHAMIRIA KUIMARISHA HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Image
Baadhi ya Viti Mwendo “Wheelchair” na Fimbo Nyeupe “White Cane” walizokabidhiwa Watu wenye Ulemavu.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Bi. Paulina Mwalimu mara baada ya kuwakabidhi vifaa saidizi hivyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TCC, Bw. Godson Killiza.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watu wenye Ulemavu waliokabidhiwa vifaa saidizi.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa hafla ya kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu iliyofanyika katika Viwanja wa Nyerere Square Jijini Dodoma. Mwakilishi kutoka Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw. Derick Amahoro akitoa maelezo kwa Waziri wa Nc...

Changudoa Afunguka ‘Nilishawahi Kulala Na Wanaume 5000’

Image
Msichana ambae anadai kuwa yeye ndie malikia wa machangudoa nchini Ghana ameweka wazi kuwa amewahi kulala na zaidi ya wanaume 5000 ili kupata pesa ambazo zilimsaidia kuishi maisha ya kifahari. Amedai kuwa watu wengi wamekua wakikosa imani nae kwakua alikua ananukia miti shamba kutoka nchi Ivory Coast ambazo alikua anapaka kwenye sehemu zake za siri wakati akiwa anafanya mapenzi, anadai kuwa alikua msafi sehemu hizo. Kwa ushuhuda wake, amedai kuwa hakuweza kusikia maumivu baada ya kulala na wanaume 20 kwasababu ya dawa alizokuwa anatumia  kwani zilifanya sehemu zake za siri kuwa tight. Muhudumu huyo wa zamani wa club anadai wengi aliowahi kulala nao walikua wanamlalamikia juu ya wake zao kuwa wachafu. Mama huyo wa machangudoa amefunguka kuwa alikua anavaa smart na kuwa msafi muda wote na wateja wake (boyfriends) wakiwa wanakuja wanamkuta msafi . Kwa maoni yake, baadhi ya wanawake waliolewa ndio wanawapa wanaume sababu za kuwasliti kutokana na tabia zao, nakuongeza...

KIMENUKA..6 Mbaroni Kwa Kugushi Vyeti Kujiunga na JKT

Image
Vijana 6 Mkoani Njombe wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kugushi vyeti katika zoezi la usahili wa kujiunga nafasi za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Hayo yamesemwa Jana Juni 29 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka alipokutana na waandishi wa habari Mkoani humo ambapo amebainisha kuwa, hatua hiyo ni maamuzi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambao wamekubaliana, kutengua Mchakato mzima wa zoezi hilo ili kuanza upya kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Haki. Olesendeka amesema, kutokana na vitendo vya udanganyifu ikiwemo kugushi uraia, wajumbe wakamati hiyo wametengua uteuzi wa nafasi za vijana waliotarajiwa kujiunga na Jeshi hilo kwa ajili ya Mafunzo. “Baada ya kupitia wilaya moja baada ya nyingine, tumebaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti kwa ikiwemo vyeti vya kuzakiwa, vyeti vya elimu ya msingi, na hata kuwepo ya viashiria kwamba, wengine Uraia wao una mashaka,” alisema Olesendeka. Alisema wamelazimika kufanya maamuzi ya kutengua uteuz...

Sakata la Tundu Lissu: Askofu Bagonza Amesema Kuna Tofauti ya Bunge na Bonge

Image
Sakata la Lissu: Askofu Bagonza amesema kuna tofauti ya Bunge na bonge Posted On: June 30, 2019 4:28 Am GMT+0000  Posted By: Beatrice Shayo  Comments: 0 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza ametoa kauli yenye fumbo kufuatika sakata la kuvuliwa Ubunge aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook alifafanua tofauti ya Bunge na bonge. Ujumbe huo wenye kichwa cha habati ‘Kuna tofauti kati ya Bunge na Bonge.’ “Bunge huongozwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni, tamaduni za mabunge, mila na desturi nzuri, busara na hekima. Askofu Bagonza aliongezea kuwa:”kikikosekana kimoja hapo juu, linageuka kuwa bonge. Maana yake, bonge linatisha, linaonea, linapendelea, linajichanganya, linahujumu, linajihujumu, linalipiza kisasi, linakera na halina utu wala huruma.” “Bunge letu siyo bonge. Mungu Ibariki Tanzania. Libariki Bunge letu. Liepushe na ma...

Mbowe: Ndugai Chukua viti Vyote Nani Mwenye Shida ya Ubunge Sisi Tunawahitaji Wananchi

Image
Kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe imekuja siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutangaza kumvua ubunge mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Akizungumza katika kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika Kanda ya Nyasa, Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni amesema hatua hiyo haiwezi kuwavunja moyo bali inazidi kuwaimarisha hata kama wabunge wao wote wataondolewa “Spika leo anamfukuza ubunge Lissu anadhani tutalia, tunamwambia Mheshimiwa Spika acha Lissu chukua viti vyote hivi, nani ana shida na ubunge, sisi tuna shida na wananchi,” amesema Mbowe. Aidha, amesema uamuzi huo umewapa hasira ambazo watazihamishia katika kuhakikisha wanaingiza wabunge wengi zaidi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuondoa wingi wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi. Akizungumza bungeni Ndugai amesema kuwa amemtaarifa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi k...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 30 June

Image
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 30 June from UDAKU SPECIAL BLOG

SIASA NA ITIKADI ZAKE VISIRUHUSIWE SANA KUINGILIA MICHEZO

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa mwisho wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 dhidi ya Algeria kesho kukamilisha ratiba na kusaka heshima. Hiyo ni baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Kenya katika mchezo wake wa pili wa Kundi C Alhamisi wiki hii Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo. Baada ya kufungwa 2-0 na Senegal kwenye mchezo wa kwanza Juni 23, sasa Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria Julai 1 kukamilisha ratiba na kusaka heshima, wakati Kenya itahitaji ushindi mbele ya Senegal kuangalia uwezekano wa kusonga mbele kufuatia kupoteza mechi ya kwanza. Alhamisi ya Juni 27, kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Happygod Msuva alianza kuifungia Taifa Stars bao zuri na la mapema dakika ya sita tu ya mchezo. Lakini mshambuliaji wa Kashiwa Reysol ya Japan aliyewahi kuchezea Girona ya Hispania kwa mkopo, Michael Ogada Olunga aliisawazishia Harambee Stars kwa tik tak dakika ya 39 akitumia makosa...

MAGAZETI YA LEO 30/6/2019

Image
from MUUNGWANA BLOG