Mbowe: Ndugai Chukua viti Vyote Nani Mwenye Shida ya Ubunge Sisi Tunawahitaji Wananchi


Kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe imekuja siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutangaza kumvua ubunge mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akizungumza katika kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika Kanda ya Nyasa, Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni amesema hatua hiyo haiwezi kuwavunja moyo bali inazidi kuwaimarisha hata kama wabunge wao wote wataondolewa

“Spika leo anamfukuza ubunge Lissu anadhani tutalia, tunamwambia Mheshimiwa Spika acha Lissu chukua viti vyote hivi, nani ana shida na ubunge, sisi tuna shida na wananchi,” amesema Mbowe.

Aidha, amesema uamuzi huo umewapa hasira ambazo watazihamishia katika kuhakikisha wanaingiza wabunge wengi zaidi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuondoa wingi wa wabunge wa Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza bungeni Ndugai amesema kuwa amemtaarifa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi kwakuwa aliyekuwa Mbunge wake, Lissu amevunja taratibu na kanuni kwa kutohudhuria vikao kadhaa vya bunge bila kutoa taarifa na kushindwa kujaza fomu ya maadili.

Ndugai amesema amekuwa akimuona kwenye vyombo vya habari akizunguka nchi mbalimbali na kufanya mikutano lakini hahudhurii vikao vya bunge wala kutoa taarifa zenye sababu ya kutohudhuria vikao hivyo, kinyume cha kanuni na sheria husika

from UDAKU SPECIAL BLOG

Comments

Popular posts from this blog