ALAIN OLIVER NIYUNGEKO- MPENI MUDA ZAIDI MAVUGO ILI MFAIDI MATUNDA YAKE
Mavugo alianza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za awali baada ya kujiunga na Simba halafu akapotea na akaanza kuwekwa benchi lakini baadae akaibuka Kocha mkuu wa Burundi Alain Oliver Niyungeko amesema klabu ya Simba inatakiwa kumpa muda zaidi mshambuliaji wao Laudit Mavugo ili wavune mambo mazuri kutoka kwa nyota huyo Niyungeko alisema Mavugo ni mchezaji mwenye kipaji cha pekee hivyo kuanza vibaya kwenye msimu wa kwanza hawapaswi kumwonyesha mlango wa kutokea bali wampe muda ili aweze kuzoea mazingira. “Mavugo kule nyumbani Burundi ndiye mshambuliaji tishio, ambaye achana na huyu Amissi Tambwe ambaye nasikia huku ndiyo mkali wa mabao na mabadiliko ya mazingira ndiyo yanayochangia mchezaji kufanya vibaya lakini wanapaswa kumpa muda,”amesema Niyungeko. Kocha huyo amesema endapo Simba wataamua kuachana na mchezaji huyo wanaweza kujutia maamuzi yao kwani mchezaji huyo bado hajatokea mfano wake nchini Burundi na hata Afrika Mashariki. Amesema mshambuliaji huyo anafaida nyingi ku...