VILABU VITATU UJERUMANI VINAMUITAJI SAMATTA, GENK YAWEKA BEI YAKE


Vilabu vitatu vya Ligi ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga vinamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta.
Kwa mujibu wa wakala anayeishi Ubelgiji makachero wa timu za Wolfsburg, Hamburger SV na Borussia Mönchengladbach wamekuwa wakimfuatilia Samatta anayetajwa kuwekewa thamani ya euro milioni 10.
Klabu ya Genk inasemekana iko tayari kumuachi Samatta mwenye mkataba hadi mwaka 2020 kwa dau lisilopungua euro milioni 10 licha ya kumnunua kwa Euro 800,000 kutoka klabu ya TP Mazembe mwanzoni mwa mwaka jana.

Comments

Popular posts from this blog