ALAIN OLIVER NIYUNGEKO- MPENI MUDA ZAIDI MAVUGO ILI MFAIDI MATUNDA YAKE



Mavugo alianza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za awali baada ya kujiunga na Simba halafu akapotea na akaanza kuwekwa benchi lakini baadae akaibuka

Kocha mkuu wa Burundi Alain Oliver Niyungeko amesema klabu ya Simba inatakiwa kumpa muda zaidi mshambuliaji wao Laudit Mavugo ili wavune mambo mazuri kutoka kwa nyota huyo
Niyungeko alisema Mavugo ni mchezaji mwenye kipaji cha pekee hivyo kuanza vibaya kwenye msimu wa kwanza hawapaswi kumwonyesha mlango wa kutokea bali wampe muda ili aweze kuzoea mazingira.
“Mavugo kule nyumbani Burundi ndiye mshambuliaji tishio, ambaye achana na huyu Amissi Tambwe ambaye nasikia huku ndiyo mkali wa mabao na mabadiliko ya mazingira ndiyo yanayochangia mchezaji kufanya vibaya lakini wanapaswa kumpa muda,”amesema Niyungeko.

Kocha huyo amesema endapo Simba wataamua kuachana na mchezaji huyo wanaweza kujutia maamuzi yao kwani mchezaji huyo bado hajatokea mfano wake nchini Burundi na hata Afrika Mashariki.
Amesema mshambuliaji huyo anafaida nyingi kutokana na uzoefu wa mechi za kimataifa na pia ni mchezaji ambaye analijua vizuri goli pindi anapoachiwa nafasi ya kufanya maamuzi anapokuwa uwanjani.
“Mavugo ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, aliwahi kuwa mfungaji bora kwenye ligi ya Burundi hata kwenye timu ya taifa amekua akifanya vizuri pia mara kwa mara kwahiyo sioni haja ya Simba kuhofia kiwango chake kwasababu bado anamuda wa kurekebisha makosa yake kutokana na umri aliokuwa nayo.” amesema.
“Unapojiunga na timu mpya kwenye ligi mpya wakati mwingine unahitaji muda ili kuzoea, unapokutana na wachezaji wapya kocha mpya na falsafa mpya wakati mwingine inakua vigumu kufanya vizuri mapema hivyo inabidi upate muda wa kuzoea.”
Mavugo alianza kwa kufanya vizuri kwenye mechi za awali baada ya kujiunga na Simba halafu akapotea na akaanza kuwekwa benchi lakini baadae akaibuka tena na kuanza kufanya vizuri na kurudi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog.
Simba walipanga kuachana na mchezaji huyo kwenye dirisha dogo la msimu huu, lakini baadaye walibadili mawazo yao na kumpa nafasi ya mwisho mchezaji huyo ambaye sasa ameanza kurudisha matumaini baada ya kuanza kufanya kazi ambayo ilikuwa inatarajiwa kutoka kwake.

DOWNLOAD APP YETU YA NIJUZEHABARI HAPA USIPITWE NA CHOCHOTE KILE TUNAWEKA HAPA

Comments

Popular posts from this blog