TETEZI ZA USAJILI KUTOKA BARANI ULAYA LEO TAR 31 JANUARY 2017
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele, 20, lakini huenda mabingwa hao wa Scotland wasiwe tayari kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa Under-21 chini ya paundi millioni 40. (Chanzo Sky Sports) Celtic wamekuwa wagumu kumuuza Dembele. (Chanzo Daily Record) Chelsea wanajaribu kuharakisha mpango wa kumsajili beki wa Schalke na timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac, 23, baada ya beki wao wa Serbia Branislav Ivanovic, 32, kukubali kujiunga na Zenit St Petersburg. (Chanzo Mirror) West Brom watatoa dau la paundi millioni 10 kwa mshambuliaji wa Southampton na England Jay Rodriguez, 27. (Chanzo Express) Crystal Palace wameongeza jitihada zao za kumsaka beki wa Liverpool Mamadou Sakho, 26, na wanaamini watakamilisha dili la kumpata mchezaji huyo wa Ufaransa siku ya leo ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili. Palace wanataka kukamilisha pia dili la kumsajili kiungo wa Serbia Luka Milivojevic, 25, kutoka Olympiakos na beki wa Uruguay Martin Caceres, 2...