TETEZI ZA USAJILI KUTOKA BARANI ULAYA LEO TAR 31 JANUARY 2017
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele, 20, lakini huenda mabingwa hao wa Scotland wasiwe tayari kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa Under-21 chini ya paundi millioni 40. (Chanzo Sky Sports)
Celtic wamekuwa wagumu kumuuza Dembele. (Chanzo Daily Record)
Chelsea wanajaribu kuharakisha mpango wa kumsajili beki wa Schalke na timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac, 23, baada ya beki wao wa Serbia Branislav Ivanovic, 32, kukubali kujiunga na Zenit St Petersburg. (Chanzo Mirror)
West Brom watatoa dau la paundi millioni 10 kwa mshambuliaji wa Southampton na England Jay Rodriguez, 27. (Chanzo Express)
Crystal Palace wameongeza jitihada zao za kumsaka beki wa Liverpool Mamadou Sakho, 26, na wanaamini watakamilisha dili la kumpata mchezaji huyo wa Ufaransa siku ya leo ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili. Palace wanataka kukamilisha pia dili la kumsajili kiungo wa Serbia Luka Milivojevic, 25, kutoka Olympiakos na beki wa Uruguay Martin Caceres, 29. (Chanzo Daily Mail)
Watford wamekubali dau la paundi millioni 20 kutoka klabu ya Changchun Yatai ya Chinese Super League lililotolewa kwa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 27. (Chanzo Sun)
Winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco – ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United na Chelsea – inasemekana hana wakati mzuri hapo Atletico Madrid, huku taarifa zikidai kuwa kumekuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na kocha Diego Simeone. (Chanzo Don Balon, kupitia Manchester Evening News)
West Ham imetishia kufuta dili la paundi millioni 25 la kumuuza Dimitri Payet, 29, kwa Marseille ikiwa mchezaji huyo wa Ufaransa hatorudisha mshahara wa paundi 500,000 wa mwezi huu Januari. (Chanzo London Evening Standard)
Haya, Leo ndio siku ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi huu Januari na hayo ndio machache tuliyokutayarishia kutoka hapa nijuzehabari.com,
Comments
Post a Comment