BASTIAN SCHWEINSTEIGER BADO YUPO YUPO MANCHESTER UNITED

Bastian Schweinsteiger hataihama klabu ya Manchester United na atajumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kinachocheza ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, kwa mujibu wa meneja Jose Mourinho.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga wakati wa ushindi wa United wa 4-0 Kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili.

Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016.
Schweinsteiger aliachwa nje ya kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho na akalazimishwa kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 mwanzoni mwa msimu.
Msimamo wa ligi ya EPL 2016/17
Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young

"Ataenda kucheza Europa League kwa sababu tumeachwa na nafasi za kujaza kutokana na kuondoka kwa [Memphis] Depay na [Morgan] Schneiderlin."
Schneiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye.
United watakutana na Saint-Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16 Februari, na mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye.

Comments

Popular posts from this blog