TETESI ZA USAJILI KUTOKA BARANI ULAYA TAR. 30 JANUARY 2017
Beki wa Chelsea kutoka nchini Serbia Branislav Ivanovic, 32, yuko karibuni kukubaliana mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya Urusi Zenit St Petersburg. (Chanzo Daily Mail)
West Bromwich Albion watatoa dau kumbakisha Branislav Ivanovic katika Ligi Kuu Uingereza. (Chanzo Daily Mirror)
Coleen Rooney amemruhusu mumewe mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 31, kuchukua ofa ya paundi 140 ya kwenda kucheza China. (Chanzo Daily Star)
Sunderland wanajiandaa kutoa dau kwa mshambuliaji wa Leicester na Argentina Leonardo Ulloa, 30. (Chanzo Chronicle)
Bosi wa Sunderland, David Moyes atatoa dau la paundi millioni 11 kwa Ulloa. (Chanzo Sun)
Leicester inataka kumsajili beki wa Anderlecht kutoka nchini Senegal Kara Mbodji, 27 pamoja na kiungo wa Middlesbrough kutoka nchini Uruguay Gaston Ramirez, 26. (Chanzo Leicester Mercury)
Newcastle na Crystal Palace wanajidili uwezekano wa kubadilishana wachezaji ambapo tunaweza tukaona winga wa England Andros Townsend, 25, akarejea Newcastle, na Beki kutoka nchini DR Congo Chancel Mbemba, 22, akaelekea Crystal Palace. (Chanzo Sky Sports)
Liverpool bila shaka hawatafanya usajili wa mchezaji yoyote kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la mwezi huu Januari, licha ya kuhusishwa na kiungo wa Roma na timu ya taifa ya Argentina Leandro Paredes, 22. (Chanzo Liverpool Echo)
Golikipa wa Chelsea kutoka nchini Bosnia Asmir Begovic, 29, amethibitisha nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo na anasema “amepoteza muda” akisugua benchi hapo Stamford Bridge. (Chanzo Daily Mirror)
Usikose kufatilia habari kama hizi kila siku kwa kuja kwenye blog yetu pendwa ya nijuzehabari.com tunawatakia Siku njema
Comments
Post a Comment