Posts

Showing posts from April, 2019

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA DANNY MRWANDA

Image
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

BIASHARA UNITED 0-2 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

MESSI AIPA BARCELONA TAJI LA NANE LA LIGA NDANI YA MIAKA 11

Image
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao pekee dakika ya 62 ikiilaza Levante 1-0 Uwanja wa Camp Nou na kujihakikishia taji la pili mfululizo la La Liga na la nane ndani ya misimu 11   PICHA ZAIDI GONGA HAPA from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

WAKALI WA NDOVU YA ARUSHA 1992, RASHID CHAMA, KABURU NA LUNGU

Image
WACHEZAJI wa Ndovu ya Arusha kutoka kulia kiungo mshambuliaji Francis Lungu (sasa marehemu), beki Rashid Idd ‘Chama’ na kiungo Abdallah Suleiman ‘Kaburu’ kabla ya moja ya mechi za timu hiyo mwaka 1992 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

SAMATTA AISAIDIA KRC GENK KUIBUKA NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA KAA GENT UBELGIJI

Image
Na Mwandishi Wetu, GENT MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amesaidia klabu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent. Samatta jana alisababisha tu bao hilo pekee lililofungwa na mshambuliaji mwenzake tegemeo la timu hiyo, Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya 55 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy. Kwa ushindi huo Samatta sasa anakaribia kabisa kuipa taji la ubingwa wa Ligi ya Ubelgiji Genk, kwani inazidi kupaa kileleni kwenye hatua ya mwisho ya ligi hiyo. Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana ameichezea Genk mechi yake ya 152 akiwa ameifungia mabao 61 kwenye mashindano yote tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 119 sasa na kufunga mabao 46 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na...

MSUVA APIGA ZOTE MBILI DIFAA HASSAN EL-JADIDI YAICHAPA MOGHREB TETOUAN 2-0 MOROCCO

Image
Na Mwandishi Wetu, CASABLANCA WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga mabao yote mawili timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Moghreb Tetouan katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan. Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaam alifunga mabao yake hayo dakika za 63 na 73 na kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo inayotumia jezi za rangi ya kijani na nyeupe. Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El –Jadidi inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya nane kwenye msimamo wa Botola Pro inayoshirikisha timu 16. Simon Msuva (kulia) akishangilia baada ya kufunga mabao yote mawili Difaa Hassan El-Jadidi ikishinda 2-0 dhidi ya Moghreb Tetouan   Vigogo Wydad Casablanca waliopo Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndio wanaongoza ligi hiyo kwa pointi zao 53 za mechi 25, wakifuatiwa na Raja Casablanca wenye pointi 47 za mechi 25 pi...

KMC 1-2 SIMBA SC (LIGI KUU YA TANZANIA BARA)

Image
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

‘KAPTENI’ BOCCO APIGA ZOTE MBILI SIMBA SC YAITANDIKA BIASHARA UNITED 2-0 MUSOMA

Image
Na Mwandishi Wetu, MUSOMA SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Shujaa wa Simba SC leo ni Nahodha wake, mshambuliaji John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza. Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Patrick Aussems inafikisha pointi 69 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Yanga SC wenye pointi 74 za mechi 32. Bocco, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, alifunga mabao yake yake yote akimalizia kazi nzuri ya beki Mghana, Asante Kwasi la kwanza dakika ya 33 kwa shuti baada ya pasi ndefu na la pili kwa kichwa akimalizia krosi kutoka upande wa kushoto. Refa Ally Simba kutoka Geita alimtoa kwa kadi nyekundu kiungo Mnyarwanda wa SImba, Haruna Niyonzima dakika ya 71 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kwa kumtolea ...

RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE RUNGWE NA KYELA MKOANI MBEYA

Image
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli akisalimia wananchi wa Busokelo wilayani Rungwe katika mkoa   wa Mbeya wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika. Pamoja naye ni Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli akihutubia wananchi wa Busokelo wilayani Rungwe katika mkoa  wa Mbeya wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika. Pamoja naye ni Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila (kulia).   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Po...

WCF YASHINDA TUZO KATIKA MASWALA YA AFYA NA USALAMA MAHALA PA KAZI JIJINI MBEYA

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Tuzo na Cheti Bw. Masha Mshomba Mkurugenzi Mkuu wa WCF. Mfuko umekuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani, 2019. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Siku ya Afya na Usalama Duniani Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary jijini Mbeya.   Tuzo na Cheti katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani, 2019. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama(wa kwa...

TIMUN 2019 YAANZA RASMI MORO

Image
MKUTANO kivuli wa Baraza la Umoja wa mataifa (TIMUN2019) umeanza Jana tarehe 29/4/2019 katika mji wa Morogoro, kiasi cha kilometa 192 kutoka mji wa kibiashara wa Dar es salaam. Mkutano huo ambao unahudhuriwa na vijana 200 kutoka duniani kote unafanyika chini ya kaulimbiu "Sauti za Vijana kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu: Uwezeshwaji Ujumuishwaji na Usawa." Afisa wa Habari katika kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)  Bi. Nafisa Didi akizindua rasmi mwanzo wa mkutano kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa alihimiza vijana kutumia vizuri muda wao katika mkutano huu wa siku tano na kuonyesha vipaumbele vinne muhimu vya kujadiliwa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia (SDGs). Mkutano huo mkubwa unaendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kisheria na kikanuni. Mkutano huo unatambuliwa kimataifa kama Tanzania International Model United Nations (TIMUN) 2019 unajumuisha vijana kuanzia miaka 15-30. Kwa mujibu wa taarifa majad...