SAMATTA AISAIDIA KRC GENK KUIBUKA NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA KAA GENT UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu, GENT
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amesaidia klabu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Ghelamco-Arena mjini Gent.
Samatta jana alisababisha tu bao hilo pekee lililofungwa na mshambuliaji mwenzake tegemeo la timu hiyo, Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya 55 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy.
Kwa ushindi huo Samatta sasa anakaribia kabisa kuipa taji la ubingwa wa Ligi ya Ubelgiji Genk, kwani inazidi kupaa kileleni kwenye hatua ya mwisho ya ligi hiyo.

Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana ameichezea Genk mechi yake ya 152 akiwa ameifungia mabao 61 kwenye mashindano yote tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 119 sasa na kufunga mabao 46 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili na Europa League amecheza mechi 24 na kufunga mabao 14.
Kikosi cha AA Gent kilikuwa; Kaminski, Souquet, Verstraete, Odjidja/Bezus dk65, Sorloth, Kvilitaia/David dk57, Dejaegere, Asare/De Smet dk76, Bronn, Esiti na Derijck.
KRC Genk; Vukovic, Uronen, Lucumi/Aidoo dk52, Dewaest, Maehle, Berge, Malinovskyi, Heynen, Trossard, Ito/Paintsil dk90+2 na Samatta.


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

Comments

Popular posts from this blog